"... serikali inapotoa fedha inahitaji utekelezaji, tuzingatie muda wa ukamilishaji wa miradi yetu ya maendeleo ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita tusifurahie kuona miradi ikichelewa kukamilika..." DC Ngubiagai.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cde. Christopher Ngubiagai katika muendelezo wa ziara zake za ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kata ya Bukanda, Bukongo na Kagunguli lengo likiwa kuona uendelevu wa utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka mafundi kuongeza kasi.
Amewaasa wataalam hao kutimiza majukumu yao na kushirikisha mamlaka husika ili kutokukwamisha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.
Miradi iliyotembelewa ni ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara katika shule ya sekondari Bukanda yenye thamani ya shilingi milion 60,000,000 fedha kutoka serikali kuu, ujenzi wa shule mpya ya msingi katika kata ya Bukanda ambapo serikali imetoa milioni 330,700,000 kupitia mradi wa BOOST.
Katika kata ya Bukongo na Kagunguli miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Mwitongo ambapo shilingi milioni 63,600,000 imetolewa, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya msingi Murunazi iliyopo kijiji cha Kagunguli shilingi milion 101 fedha kutoka serikali kuu imetolewa kupitia mradi wa programu ya BOOST.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.