Serikali kupitia Wakala wa Umeme na Ufundi Tanzania (TEMESA) inaendelea na zoezi la kawaida kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto kwa taasisi mbalimbali za umma ambapo Januari 21,2026 ilikuwa zamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
Zoezi linatekelezwa na wataalam wa TEMESA kupitia karakana inayotembea, lengo likiwa kuboresha usalama wa vyombo vya moto kwa kuvikagua,kugundua changamoto zake na kuzipatia ufumbuzi sambamba na kutoa ushauri kwa madereva namna ya kuvitunza na kuwafundisha wateja wao Mfumo Unaosimamia Magari serikalini (MUM).
Jumla ya vyombo vya moto 24 vya Halmashauri na baadhi ya taasisi za serikali ndani ya Ukerewe vimefanyiwa ukaguzi .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.