Zoezi la kupokea watumishi ajira mpya 2026 linaendelea vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndugu Vincent Augustino Mbua anatoa shukrani za dhati kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta jumla ya watumishi 152 wa kada mbalimbali za afya,elimu,kílimo, mawasiliano, ujenzi na miundo mbinu,mifugo, biashara, mazingira, maendeleo ya jamii,utamaduni na uvuvi ambapo hadi sasa zoezi la mapokezi limefikia 60% .
Ongezeko hili litaleta nafuu na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza kasi ya matokeo chanya .
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.