• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Ukerewe District Council
Ukerewe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
        • Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
        • Ustawi wa Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Utamaduni ,sanaa na michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Maji
    • Uvuvi
    • Kilimo na Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Ongoing Projects
    • Miradi Iliyo kamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Sheria Ndogondogo za Halmashauri
    • Fomu za Maombi
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa kwa Umma
    • Video

WANANCHI WAASWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA WANYAMA HATARISHI

Posted on: January 23rd, 2026

Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira inaendelea kuwaasa wananchi wake kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hatarishi kama vile mamba,viboko na nyoka wanaopatikana kwa wingi kando kando ya vyanzo vya maji.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngoma ambapo wamekuwa wakidhibiti wanyama pori aina ya mamba mara kadhaa Afisa wanyama pori wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndugu Zebedayo Timotheo amewaasa wananchi kuchukua tahadhari katika maeneo hatarishi yenye viashiria vya uwepo wa wanyama hao kwa kuzingatia kuwa Ukerewe ni kisiwa na wengi wao wanapatikana kwenye maji.

Sambamba na elimu ya kujilinda dhidi ya wanyama hatarishi Afisa wanyama pori amesema kitengo cha maliasili kinaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na wanyamapori hao ikiwemo kutoa elimu ya uhifadhi endelevu,elimu ya kujikinga na kujilinda dhidi ya wanyama hatarishi, kufanya doria za mara kwa mara,ujenzi wa vizimba (crocodile enclosure) kwa ajili ya kupunguza migongano baina ya wanyama pori na wananchi.

Goodluck J.Mtigandi ni Mkuu wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira Ukerewe yeye amewaasa wananchi wanaojishughulisha na uvuvi kutumia vyombo salama na sahihi na wapende kwenda maeneo ya ziwa kwa makundi hasa nyakati za jioni,usiku na asubuhi sana huku akitoa pole kwa wahanga wote walioathiriwa na wanyamapori hao kwa namna mbalimbali.

Julius Magoma ni mkazi wa kijiji cha Nantare anaushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kwa ushirikiano mzuri na wananchi kwa kuwa wepesi kufika kwenye eneo la tukio punde wanapopata taarifa ya uwepo wa wanyama hatarishi.

Ikumbukwe kwamba tayari wananchi wawili ndani ya mwaka huu 2026 wamepoteza maisha kwa kujeruhiwa na mamba ndani ya kata ya Ngoma katika kijiji cha Nantare na Muluseni.

Matangazo

  • NAMNA YA KUOMBA LESENI ZA BIASHARA KUPITIA MFUMO WA TAUSI September 17, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JKT- UKEREWE January 22, 2026
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TIMU YA MENEJIMENTI YAKAGUA MIRADI

    February 03, 2026
  • DC NGUBIAGAI AWAASA WANANCHI KUTUMIA NJIA HALALI KUTAFUTA HAKI

    February 02, 2026
  • " BARAZA LA MADIWANI NI KIOO CHA UONGOZI KWA WANANCHI " - DC NGUBIAGAI

    January 28, 2026
  • " TUMEWAPOKEA AJIRA MPYA WETU KWA 100% - MKURUGENZI MBUA

    January 29, 2026
  • Angalia Zaidi

Video

FURSA ZA UWEKEZAJI UKEREWE
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • https://www.moe.go.tz/sw/article/tangazo-la-nafasi-za-mafunzo-ya-ualimu-ngazi-ya-astashahada-ya-ualimu-elimu-ya-awali-msingi-na-stashahada-ya-ualimu-elimu-sekondari-sayansi-miaka-mitatu-kwa-mwaka-wa-masomo-20222023
  • Jiwe linalocheza Wilayani Ukerewe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

Tovuti Mashuhuri

  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Necta

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.