Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe wametakiwa kuwa wazalendo katika masuala yote ya usimamizi wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa wilayani humo.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Vincent Augustino Mbua wakati wa kikao kazi na maafisa elimu kata, watendaji wa kata, waganga wafawidhi na wakuu wa idara mbalimbali zinazohusika na masuala ya ujenzi, manunuzi, Afya,elimu na maendeleo ya jamii.
" Serikali imetoa fedha nyingi kupitia miradi mbalimbali ya BOOST,SWASH,WASH,GPE-TSP na fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ndani ya Wilaya yetu,tuonyeshe shukrani na uzalendo katika kusimamia miradi hiyo kwa uadilifu.Ni matamanio yangu kuona miradi inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha walengwa" amesema
Mkurugenzi Mbua amewataka wataalam hao kuwabaini wazabuni wasumbufu na kuacha kuwapa tenda huku akiwasihi kufanya kazi kwa bidii na kuweka kando maslahi binafsi.
Nae mwakilishi wa Afisa elimu msingi ndugu Rasuli Amiri amewasihi wataalam hao kufahamu miongozo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili utekelezaji uwe wa viwango vya ubora vinavyokubalika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.