Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe limekaa kikao maalumu kujadili bajeti ya mwaka 2019/2020 na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo za mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inategemea kukusanya na kutumia takribani Tshs. bilioni 42 kutoka vyanzo vya ndani, serikali kuu na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kawaida na miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mhe. George Nyamaha amewataka wakuu wa idara na vitengo kufanyia kazi ushauri na maelekezo yaliyotolewa na waheshimiwa madiwani katika kikao hiko na kuongeza juhudi za makusudi katika kuongeza mapato ya Halmashauri.
Nyamaha amewapongeza Mkuu wa Wilaya Mhe. Cornel Magembe kwa kuwa amekua mstari wa mbele kuhakikisha kila kijiji kina mradi wa maendeleo na hii inaenda sambamba na kujibu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema Nyamaha. Aidha aliongeza kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Bi. Ester A. Chaula kwani amebadilisha menejimenti na kazi zinafanyika.
Amewataka madiwani kwenda na kasi ya kuhimiza maendeleo katika maeneo yao ambapo amewataka wawepo katika maeneo yao ili wahimize maendeleo kwani wao ndio wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.