IJUE IDARA YA ELIMU MSINGI –UKEREWE
Idara ya Elimu Msingi ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
Idara hii ndiyo yenye jukumu kubwa la kuhakikisha wanafunzi,watoto wenye mahitaji maalumu na watu wazima katika jamii ya Ukerewe wanapata Elimu iliyo bora kwa kizazi kilichopo na kijacho, kwani Elimu ndiyo Ufuguo wa maisha kwa jamii inayopenda maendeleo.
Idara hii inaundwa na vitengo vya Taaluma,Vifaa na takwimu na Elimu ya watu wazima ikishirikiana kwa karibu sana na kitengo cha TSD na Udhibiti Ubora wa Elimu.
SHUGHULI MBALI MBALI ZINAZOFANYIKA NA IDARA HII
Kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu na mafunzo ,sheria na Kanuni zinazoongoza elimu ya awali na msingi.
Kutoa ushauri wa kitaaluma kuhusu utoaji wa Elimu ya awali na msingi kwa mkurugenzi Halimashauri.
Kuratibu upanuzi wa elimu katika ngazi ya elimu ya Awali,EWW ,Vituo vya ufundi standi na elimu maalumu.
Kuhakikisha kwamba shule zote zinainua ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Halmashauri ya Wilaya.
Kukusanya,kuratibu na kuchambua takwimu za Elimu katika Halmashauri kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika ngazi ya shule,Halmashauri,Mkoa na Taifa.
Kusimamia shughuli za maendeleo ya taaluma Wilayani.
Kufatilia utekelezaji taarifa za wadhibiti ubora wa shule na kuishauri Halmashauri mbinu za kuinua taaluma ,Michezo na ubora wa Elimu
Kusimamia Udhibiti wa nidhamu ,Wajibu,haki na huduma za walimu na wanafunzi .Kwa kesi za walimu wanashirikiana na TSD.
MALENGO YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.