IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
UTANGULIZI:
Idara ya ardhi na maliasili ina sekta mbili ambazo ni sekta ya ardhi na sekta ya maliasili.
Sekta ya ardhi ina watumishi tisa (9) wa kada mbalimbali zinazohusu ardhi. Sekta hii hushughulika na mambo yafuatayo;
MISITU
Sehemu hii ina watumishi watano (5) pamoja na mmoja kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Wilaya ya Ukerewe ina misitu mitano (5) iliyohifadhiwa. Kati ya hiyo msitu mmoja (Rubya) unamilikiwa na Serikali Kuu na una ukubwa wa hekta 1926. Misitu minne (4) inamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ambayo ni
Kabingo LAFR hekta 250
Itira LAFR hekta 109
Mkigagi LAFR hekta 116.15
Negoma LAFR hekta 697.7
Mnamo tarehe Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe iliingia makubaliano na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya uendelezaji wa misitu minne tajwa hapo juu.
Shughuli zinazofanywa kwenye sekta misitu ni;
WANYAMAPORI
Sehemu hii ina mtumishi mmoja ambaye kazi yake ni kuhifadhi wanyamapori na kuhakikisha hawafanyi uharibu kwenye maeneo ya wananchi.
Idara inafanya kazi kwa kushirikiana na idara zingine ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.