UTANGULIZI
Idara ya Kilimo inaundwa na sehemu tatu ambazo ni Mazao, Umwagiliaji na Ushirika. Idara hii ndiyo ina jukumu la kuhakikisha Wilaya inazalisha mazao ya chakula na biashara kwa tija na kuwa na uhakika wa chakula kwa ajili ya wananchi wote kupitia shughuli za kilimo zinazosimamiwa na Idara kwa kusaidiana na wadau wengine wa Kilimo kutoka nje na ndani ya Wilaya
Kilimo ndicho maisha ya kila siku na uchumi kwa wananchi walio wengi kwa kila dakika inayopita. Kila mtu , kila mahali katika Wilaya na hata katika nchi nzima lazima aone, ashike na afanye kitu kinachohusianna na kilimo katika mtazamo chanya au mtazamo hasi. Hii inaelezea ni kwa nini kilimo ni muhimu na uti wa mgongo wa uchumi wetu kwani kilimo ndicho kinaajiri zaidi ya asilimia 80 ya watanzania na kiasi cha asilimia 92 cha wakazi wa wilaya ya Ukerewe ambaohutegemea kilimo.
SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOFANYIKA
Mazao yalimwayo kwa wingi katika Wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 38 japo visiwa 15 vinatumika kama maeneo ya uvuvi ni muhogo, viazi vitamu, mpunga, matunda aina ya machungwa, maembe, mananasi, mapapai, kahawa, migomba, mazao ya
|
bustani na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage, njugu mawe na kunde. Mazao mengine yanayolimwa kwa kiasi kidogo ni mtama na rosella (choya). Mazao haya yanalimwa katika eneo la Ha.33, 765.5
Ardhi iliyopo ni ndogo kuruhusu kilimo cha kupumzisha mashamba. Kwa hali hiyo kilimo kinahitaji kifanyike kwa tija ili uzalishaji wa mazao uweze kukidhi mahitaji ya wananchi wote ambao kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 347,145. Zao la alizeti linatiliwa mkazo badala ya zao la pamba ambalo katika
miaka ya 1970 lilikuwa zao maarufu la biashara ambalo lilikuwa linawapatia wakulima kipato. Lakini kutokana na upungufu wa ardhi hasa ukizingatia kuwa zao hili halitakiwi kuchanganywa na mazao mengine pamoja na kushuka kwa bei, zao hili lilionekana kutofanya vizuri.
|
Idara ya Kilimo ili iweze kutekeleza vyema ilani ya Uchaguzi ya CCM ni lazima ihakikishe inatekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ili kuleta tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kuendeleza na kuboresha huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuwezesha wakulima kuwa na vyama vya ushirika vilivyo hai na vyenye nguvu ya mtaji. Aidha kuwawezesha wakulima kuunda vikundi ili waweze kuwa na umoja wenye nguvu katika kufikisha bidhaa zao katika masoko ya mazao yao. Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya Vyama Vya Ushirika 71 vilivyoandikishwa chini ya Sheria Na.6 ya mwaka 2013 ya Vyama Vya Ushirika. Idadi ya VICOBA vilivyopo ni 150. Vyama vilivyo vingi vinakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea vyama hivyo kutofanya vizuri. halmashauri inakabiliwa na upungufu wa wataalam 4 wa Ushirika kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mahesabu. Ili haya yaweze kufanyika kwa ufanisi Maafisa Ugani wanatakiwa kuboreshewa mazaingira yao ya kufanyia kazi. Maboresho hayo ni pamoja na kupatiwa nyumba za kuishi katika maeneo yao na kuwezeshwa vyombo vya usafiri hususani pikipiki ili kuwawezesha kuwafikia wakulima kwa urahisi na kwa muda muafaka pale huduma za ugani zinapohitajika.
Pamoja na Serikali kutilia mkazo juu ya kilimo cha umwagiliaji wakulima bado wanategemea mvua katika kilimo. Hii ni kutokana na kutokamilika kwa miundo mbinu ya umwagiliaji katika skimu za Bugorola na Miyogwezi. Miradi hii imekwamakukamilika kutokana na ukosefu wa fedha licha ya Ofisi hiyo ya Umwagiliaji
|
Kibanio (Head Work) katika skimu ya umwagiliaji Miyogwezi
Kanda ya Ziwa kuomba fedha mara kwa mara kutoka Serikalini kwa ajili ya kukamilisha miradi. Hata hivyo jitihada zinaendelea ambapo Halmashauri katika Bajeti ya Mwaka 2017/2018 imetenga jumla ya Tsh. 354,141,458.40 kwa ajili ya kukamilimisha mradi wa Bugorola.
|
Mashine ya kusukuma maji katika skimu ya umwagiliaji Bugorola
Upatikanaji wa takwimu sahihi za utekelezaji wa shughuli za kilimo kwa wadau wa kilimo ni muhimu sana kwa ajili ya kuandaa sera na miongozo mbalimbali. Ili kuhakikisha suala hili linatekelezwa kwa ufanisi Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) limesaidia kuandaa mfumo wa utoaji wa takwimu za kilimo kutoka ngazi ya Kata hadi Taifa kwa kutumia “internet” yaani Agricultural Routine Data System (ARDS-Web Portal). Mfumo huu unawezesha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kupata takwimu za kilimo kutoka maeneo mbalimbali kwa urahisi zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Changamoto kubwa tuliyonayo ni upungufu mkubwa wa maafisa ugani ngazi ya kijiji na kata, hivyo kupelekea baadhi ya maafisa ugani kuhudumia kata zaidi ya moja. Vyombo vya usafiri kwa maafisa ugani pia ni tatizo ili kuwafikia wakulima kwa wakati katika maeneo yao ya kilimo. Kuwepo kwa kituo kikubwa cha rasilimali za wakulima na wafugaji katika kata ya Bukindo kumesaidia wakulima na wafugaji kupata maarifa juu ya kilimo cha mazao,ufugaji bora wa mifugo, uvuvi na ufugaji bora wa nyuki kupitia vitabu mbalimbali vilivyonunuliwa kwa fedha za DADP. Aidha kituo hiki kina ukumbi mzuri kwa ajili ya mikutano, warsha na mafunzo. Kutokana na ukosefu wa maeneo kwa ajili ya kujenga vituo vya wakulima wilaya iliamua kuwa na kituo kimoja kikubwa ambacho kitahudumia wakulima wote wilayani.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.