UTANGULIZI
Idara ya Mifugo na Uvuvi iliundwa mwaka 2010. Idara hii huundwa na sekta mbili yaani sekta ya mifugo na sekta ya uvuvi.
1.0 WATUMISHI.
Idara hii ina jumla ya watumishi 26, kati ya watumishi hao watumishi 10 ni wa sekta ya Mifugo na watumishi 16 ni wa sekta ya Uvuvi.
2.0 MALENGO YA IDARA.
Kubuni na kuimarisha mbinu za utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Kuboresha mapato ya Halmashauri yatokanayo na leseni za uvuvi, ushuru wa machinjio na ukaguzi wa nyama.
Kuimarish vikundi vya utunzaji wa rasilimali ya uvuvi katika ziwa Victoria(BMU) ili Kuhakikisha rasilimali za Uvuvi zinalindwa ipasavyo katika ziwa Vitoria.
Kusimamia na kutekeleza sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 ili Kuhakikisha Uvuvi haramu unatokomezwa wilayani Ukerewe.
3.0 SEKTA YA MIFUGO.
Sekta ya Mifugo ina jumla ya mifugo kama ifuatavyo.
MIFUGO
|
IDADI
|
Ngo’mbe
|
53567
|
Mbuzi
|
31287
|
Kondoo
|
204
|
Kuku
|
256799
|
Nguruwe
|
1647
|
Mbwa
|
10992
|
Bata
|
20286
|
4.SEKTA YA UVUVI.
Sekta ya Uvuvi ina jumla ya wavuvi 16228, wenye jumla ya mitumbwi 4057.
Katika Kuhakikisha kuwa nguvu ya uvuvi ziwani inapungua, idara inahamasisha jamii kujihusisha na ufugaji wa samaki katika mabwawa. Hadi sasa kuna jumla ya mabwawa 64 na uhamasishaji wa jamii kuongeza mabwawa mengine unaendelea.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.