Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia kitengo cha maliasili na utunzaji wa mazingira inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika masuala ya utunzaji wa mazingira kwa kuanzisha bustani ya kuotesha miche kwa ajili ya upandaji miti iliyopo ofisi kuu za halmashauri lengo likiwa ni kufidia miti iliyokatwa wilayani humo na kuendelea kutunza mazingira na uoto wa asili.
Jumla ya miche 48000 imeoteshwa katika bustani hiyo yenye mchanganyiko wa miche ya miti aina ya Mikalibea, Misila na Misadulela kwa ufadhili wa fedha za tozo chini ya mfuko wa misitu Tanzania "Tanzania Forest Fund "TaFF".
Mradi ulianza kutekelezwa mwezi Agosti 2025 na hadi sasa umetumia 80% ya fedha iliyotolewa.Miche hiyo inatarajiwa kugawiwa na kupandwa katika taasisi mbalimbali zenye eneo la ukubwa usiopungua hekta moja kwa mkataba wa utunzaji na uhifadhi wa miti hiyo.
"KWA PAMOJA TUNAWAJIBIKA KUTUNZA MAZINGIRA YETU."
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.