1.0 UTANGULIZI
Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya wakazi 345,147 (Sensa 2012), kati ya hao wananchi 209,498 wanafikiwa na huduma ya maji safi katika wilaya, ambayo ni sawa na asilimia 58 kwa vijijini na Nansio mjini ni asilimia 70.
2.0 MIRADI YA MAJI INAYOTEKELEZWA KWA SASA.
Halmashauri kwa sasa inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji vijijini unaojulikana kwa jina la "Mradi wa Maji Kanzilankanda" na unatekelezwa katika vijiji 13 ambavyo ni: Igalla, Bwasa, Lutare, Kigara, Hamuyebe, Busunda, Namagondo, Buhima,Malegea Mahande, Kazilankanda, Namasabo na Muhula.Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai 2017.
Pia Halmashauri inatarajia kuweka katika mpango wake wa bajeti zijazo kufua na kukarabati miradi 7 ya zamani ambayo haifanyi kazi ambayo ni Bugorola, Bukindo, Bwisya, Bukonyo, Gallu, Muriti na Irugwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 na 2019/2020.Kukamilika kwa utekelezaji wa miradi hii kutaongeza idadi ya wakazi wanaopata huduma ya maji safi kufikia asilimia 90% kwa upande wa vijijini.Na kukamilika kwa mradi wa maji Nansio katika vijiji vya Nansio, Kagera, Nkilizya, Nakatunguru, Kakerege, Bukongo, Nebuye,Nantare Hamkoko,Bulamba na Malegea kutaongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kufikia asilimia 100%.
Hii itapelekea jumla ya wananchi wanaopata maji safi na salama katika wilaya ya Ukerewe kiujumla kufikia 95% ifikapo 2020.
3.0 DHAMIRA YETU.
Ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2020 wakazi wote wa wilaya ya ukerewe wanapata huduma ya maji safi na salama.
Tenki la maji la Lutare la ujazo wa lita 680000. Wananchi wakichota maji mojawapo ya visima vya mradi wa HESAWA
Kazi ya uchimbaji mitaro kwa ajili ya kulaza bomba ikiendelea
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.