UTANGULIZI.
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe. Idara ina jumla ya watumishi 13 wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Afisa Vijana .Wilaya ya Ukerewe ina kata 25 kati ya 7 ndio zina Maafisa Maendeleo ya Jamii.
SHUGHULI ZA IDARA.
Idara inafanya kazi kwa kushirikiana na idara zingine ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
A: UTOAJI WA MIKOPO YA WANAWAKE KUANZIA MWAKA 2006/2007 – 2009/2010 na 2014/15
Jumla ya 58 vikudi vilivyo kopeshwa kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake kutoka. mwaka 2006/07, vikundi 12, 2008/2009 vikundi 15 2009/10 vikundi 18 na 2014/15 vikundi 13 vyenye jumla ya wanawake 290
Jumla ya Mikopo iliyotolewa kwa vikundi 58 ni Tsh. 31,700,000/= toka mwaka 2006/07 hadi 2014/15.
B: VIJANA
Jumla ya vikundi vya vijana ni 3 ambao wamepatiwa kiasi cha fedha 10,000,000/=na wanajishughulisha na ufugaji wa kuku na nguruwe pamoja na upandaji miti.Pia kuna fedha ambazo zimepokelewa kiasi cha tsh 4,750,000 zimepokelewa kutoka wizara yenye dhamana ya maendeleo ya vijana kwa ajili ya kukopesha vikundi 3, utaratibu wa kuwakabidhi fedha unafanyika.
Mafunzo ya ujuzi yanatolewa kwa Vijana 87 kati ya hao ke 52 na me 35 katika fani mbalimbali kama vile ufundi umeme wa majumbani,,matengenezo ya pikipiki ,saluni, kudarizi,matengenezo ya simu , kushona nguo, upikaji wa vyakula, kuchomelea vyuma(welding), uashi, uwekaji wa vigae majumbani na kilimo cha bustani kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali Swiss contact chini ya mpango wa U Learn. Vijana hawa wamewezeshwa elimu ya ujasiriamali, stadi za maisha, uongozi wa vikundi na namna ya kujikinga na maambukizo ya UKIMWI
C: UKIMWI.
Idara inashirikiana na Idara ya Afya katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Maeneo ambayo idara ya Maendeleo ya Jamii imejikita zaidi ni:
D: USTAWI WA JAMII.
Idara ya maendeleo ya jamii, kupitia kitengo cha ustawi wa jamii inafanya shughuli zifuatazo.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.