Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe leo amefunga mafunzo ya jeshi la akiba awamu ya pili katika tarafa ya Mumbuga wilayani Ukerewe. Hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanja cha Ukuta mmoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wazazi wa wahitimu hao. Magembe amewapongeza wahatimu wote kwa kufika hatua hiyo.
Akisoma risala katika hafla hiyo mmoja wa wahitimu ametoa shukurani za dhati kwa wakufunzi wao, wageni waalikwa pamoja na wazazi wawaliohudhuria hafla hiyo. Akibainisha changamoto zinazowakabili wahitimu hao ni sare za kuvaa pindi wanapokuwa kwenye mafunzo yao.
Pamoja na changamoto hizo wahitimu haowamebainisha mafanikio mbalimbali waliyoyapata baada ya kushiriki mafunzo hayo kwa muda wa miezi minne. Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na kupata ukakamavu wa mwili nma akili, kufahamu mbinu mbalimbali za kivita na mfanzo ya uzamiaji na namna ya kuishi polini.
Kutokana na changamoto hizo wahitimu hao waneiomba Serikali kutoa mafunzo ya awamu nyingineili waweze kukomaa vizuri kivitendo. Pia wameiomba Serikali kuwapa kipaumbele katika nafasi za kazi katika jeshi, sambmba na hayi wameiomba Serikali kuandaa kambi ya jeshi la akiba ambalo litawasaidia kukaa kambini badala ya kutokea nyumbani.
Akijibu risala hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Magembe ameahidi kutekeleza ununuzi wa sare, sambamba na hilo amewahasa wahitimu hao kudumisha heshima na nidhamu mitaani na kujiepusha na vikundi visivyofaa. Pia amewaahidi wahitimu hao kuwa atashughulikia makampuni mbalimbali yanayowaajiri walinzi wasiopitia jeshi la akiba, jambo litakalowapa nafasi wahitimu wa jeshi la akiba kuajiriwa.
Magembe amewasihi wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI na maradhi mengine kwa kufuata njia za kujikinga na ugonjwa huo. “Sitarajii kusikia mmoja kati yenu amekufa kwa ugonjwa wa UKIMWI kwa maana mmefundishwa njia za kujikinga na UKIMWI na maradhi mengine” amesema Magembe. Ukakamavu mlioupata katika mafunzo haya utafanya magonjwa nyemelezi kuwa mbali na nyinyi aliongezea Magembe.
Alikadhalika Mhe. Magembe ametoa shukurani kwa wazazi wote waliowaruhusu vijana wao kujiunga na mafunzo hayo. Pia ametoa wito kwa wazazi wote kuwaruhusu vijana wao kuijiunga na mafunzo ya jeshi la akiba pale nafasi zinapotangazwa. Kwani kwa kufanya hivo watajifunza uzalendo wa taifa lao.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.