Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya ziara Katika kisiwa cha Ukara na kuzindua Kituo cha Afya Bwisya kilichojengwa kwa gharama ya Billioni 1.3 fedha ambayo katika maeneo mengine hutolewa kujenga Hospitali ya Wilaya. “Nasema Ukerewe Oyee kwa sababu mtakua na hospitali mbili za Wilaya, moja Nansio na nyingne Bwisya” Mhe Samia Suluhu Hassan.
Ameagiza Naibu waziri wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Mwita Waitara (MB) na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Doroth Gwajima kwenda kupitia vigezo vyote na hatua zote na Kituo cha Afya Bwisya kuwa Hospitali ya Wilaya.
Makamu wa Rais Ametoa Pole kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki Katika Ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV. Nyerere kilichotokea septemba 20,2018. Amewapongeza Watanzania wote waliochanga wakati wa maafa.
Makamu wa Rais ametoa Salamu za Pongezi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua nzuri ya Ujenzi wa Kituo hiko na namna wananchi wanavyoendelea na shughuli za uzalishaji kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wana Ukara kuitunza Hospitali hii kwani ni Mali yao. Hivyo ni wajibu kuitunza kama Mali yao kwani serikali imeshafanya wajibu wake wa kuwajengea Hospitali.
Serikali inafahamu Upungufu wa watumishi hapa lakini Wizara ya Afya imeandaa list ya watumishi wote wanao hitajika Hapa Bwisya na wakisha hitimu wataletwa.
Awali Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (MB) alieleza kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Huduma ya X-ray itapatikana Bwisya.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujali na ameendelea kwa kusisitiza kuwa ni furaha kama Kituo cha Afya Bwisya kitakua Hospitali ya Wilaya.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.