Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza ndugu Julius Peter na wajumbe wa kamati ya Siasa Mkoa leo wameadhimisha miaka 44 ya Chama hiko Wilayani Ukerewe ambapo wametembelea miradi miwili ya Ujenzi wa Shule Ya Sekondari Ilangala na Sekondari ya Buzegwe inayotekelezwa na wananchi pamoja na Serikali.
Malengo katika kuadhimisha miaka 44 ni kutekeleza kwa vitendo kwa kukagua utekelezaji wa ilani na kushiriki miradi ya Maendeleo.
“Tupongeze kata na Serikali kwa kuwasogezea Huduma wananchi kwa kuanzisha Sekondari hizi”.
Katika kuadhimisha miaka 44 Katibu wa CCM Mkoa pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wamekabidhi mifuko ya saruji 20 ambapo kila Shule imekabidhiwa mifuko 10 ya saruji.
“Wanufaika wakuu ni watoto wetu hivyo niwapongeze wananchi kwa juhudi hizi hakika tuendelee kuboresha miundombinu ya kusomea watoto wetu”. Alisema Peter.
Mhe. Joshua Manumbu diwani wa kata ya Igalla na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ameeleza kuwa Halmashauri kupitia kamati ya Fedha imetenga fedha ambazo zitaletwa kwa ajili ya kuongeza nguvu ujenzi wa Shule mpya zinazoendelea kujengwa ikiwemo Ilangala na Buzegwe.
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ukerewe Mhe. Alli Mambile Amewataka wana CCM kuimarisha mshikamano na wananchi waendelee washiriki katika shughuli za Maendeleo katika kata zetu
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.