Mhe. Omary Tabweta Mgumba Naibu Waziri wa Kilimo amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe na kupokelewa na viongozi wa Wilaya Kaimu Mkuu Wa Wilaya na Katibu Tawala wa Wilaya Focus Majumbi, Mbunge wa Ukerewe Mhe. Joseph Mkundi, kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Hellen Rocky pamoja na wataalamu wa Idara ya Kilimo.
Mhe. Omary Tabweta Mgumba Naibu Waziri wa Kilimo ametembelea skimu za umwagiliaji za Miyogwezi lenye hekta 120, skimu ya Bugorola lenye hekta 200. Ambapo katika skimu zote mbili hazijakamilika.
Skimu ya Miyogwezi thamani ya mradi hadi kukamilika Ulitakiwa kutumia zaidi ya Tsh. Milion 700 na mkandarasi alilipwa Tsh. Milioni 684.
Mgumba amesikitishwa na kutokukamilika kwa miradi hiyo na kutoa maelekezo.
Ameelekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Kanda ambao ndio walioluwa wasimamizi kuwasilisha taarifa ya kina kuhusu mradi huo kwani fedha nyingi zililipwa na mradi haijakamilika.
Wote waliohisika na Kutumia kinyume na mipango ya Serikali hatua za kisheria zichukuliwe juu yao. Alisema Mgumba.
Mhe. Omary Tabweta Mgumba Naibu Waziri wa Kilimo Ameelekeza Chuo cha Utafiti cha Ukiriguru wafike Ukerewe kuchunguza kwa kina juu ya magonjwa na wadudu wanaoshambulia Muhogo.
Aidha amewataka Kituo cha Udogo cha Mlingano Tanga kutuma wataalamu kufanya tafiti ya tabaka na afya ya udongo ili kubaini matatizo katika udongo na waje na majibu yakitaalamu.
Amewataka wakulima wabadilike na walime kisasa kwa kitumia mbolea kwani inatibu ardhi na Udongo. "mbolea ndio tiba inayoongeza virutubisho vilivyopungua kwenye ardhi na udongo. Mgumba.
Ametoa rai kwa Wafanyabiashara waliokomikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula kutumia fursa ya kuleta chakula Ukerewe na kuuza kwa bei nafuu.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.