Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary (MB) leo amefanya ziara ya kikazi Wilayani Ukerewe na kutemebelea na kukagua mradi wa Chuo cha Ufundi VETA mradi unaotekelezwa kata ya Bukanda kijiji cha Muhula.
Mradi huu unagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 1.6 na maandalizi ya eneo la ujenzi ulianza January 2020 na kuanza rasmi kwa ujenzi ni tarehe 2/4/2020 na unatarajiwa kukamilika tarehe 31/3/2021 na majengo yanayojengwa ni 18 yanayojumuisha nyumba 3 za watumishi, jengo la Utawala, karakana 4 zenye fani 6, mabweni 2 na jengo moja la jiko na bwalo, jengo la darasa, jengo la umeme, Mlinzi na majengo 3 ya vyoo.
Baada ya kukamilika chuo kinategemea kuwa na fani 6 ambazo ni fani ya uchomeleaji, ushonaji, ufundi magari, uashi, umeme wa majumbani, uazili na kompyuta. Mhe. Kipanga ameomba Halmashauri kuona umuhimu wa kuwaongezea veta eneo kwani chuo hiko hapo baadae kitahitaji upanuzi.
Lengo la ujenzi wa vyuo vya VETA ni kuwezesha vijana wanaomaliza kuanzia darasa la saba na kidato cha nne na hawakuweza kufanikiwa kuendelea na vijana wengine watakao kuwa wanapenda kufanya kazi za mikono Wanaweza kuingia kwenye mafunzo haya.
“Lengo kuu ni kuwa na stadi ambazo zinaendana na shughuli kuu za maeneo husika kama Uvuvi, madini na kumuwezesha mtu kuongeza ubora katika shughuli hizo za kiuchumi”. Alisema Kipanga
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe ameishukuru Serikali kwa kuleta mradi huo katika Wilaya ya Ukerewe kwani utaenda kuwa wa manufaa sana kwani ni moja ya mradi unaosubiriwa kwa hamu na wanaukerewe ili waanze kusoma kwani stadi za ufundi zinazotolewa na VETA wanaukerewe walizifuata mwanza na maeneo mengine ya nchi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.