Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel B. Magembe azindua rasmi ugawaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee katika wilaya ya Ukerewe. Uzinduzi huo wa vitambulisho vya wazee umefanyika katika kijiji cha Nansole kata ya Bukindo na kuhudhuriwa na viongozi wa Wilaya ikiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri George M. Nyamaha, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Graygor Kalala, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi, Ester A. Chaula. Takribani wazee 15,000 wanatarajiwa kunufaika na vitambulisho hivyo kwa ajili ya matibabu bure ya wazee.
Akizungumza wa wananchi wa Nansole Mwenyekiti wa Halmashauri George M. Nyamaha amewapongeza wazee wote waliojitokeza kupigwa picha ili kupatiwa vitambulisho hivyo. Ameeleza ni mpango wa Halmashauri kutekeleza matakwa ya Ilani ambapo inawataka wazee wenye miaka 60 na kuendelea kupata matibabu bure. Hivyo baraza lake lilisimamia na kuhakikisha fedha zinapatikana na kuwezesha wazee kupata vitambulisho hivyo.
Graygor Kalala Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Bukindo ameshukuru kwani wazee 99 walioandikishwa katika kijiji cha Nansole wote wanapatiwa vitambulisho hivyo vya matibabu bure kwa wazee.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Ester Chaula amesema kwa kushirikiana na idara ya afya ataendelea kuhakikisha wazee wote wenye vitambulisho hivyo wanapata matibabu kwa haraka na kwa kipaumbele pindi waendepo kutibiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha kwa kusimamia na kuhakikisha zoezi hilo linafanikwa. Huu ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na hasa katika kuhaikikisha wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 wanatibiwa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Amewataka watoa huduma wa afya wawape kipaumbele wazee kwani ni jambo la heri kwani hata ambao ni vijana sasa ni wazee watarajiwa. Aidha amewahimiza wananchi kuendelea kuchangia maendeleo na kuwataka wawemstari wa mbele kwani maendeleo ni ya Ukerewe ni yetu sote. “kuna miradi mbalimbali ya maendeleo nilianzisha ikiwemo ujenzi wa madarasa ambapo mpaka sasa madarasa 316 yamejingwa kwa nguvu ya wananchi, tushirikiane kuyajenga maboma hayo na Serikali/Halmashauri itakamilisha”. Alisema Magembe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.