Wahamiaji haramu waliopo katika maeneo ya visiwa kutoka nje ya nchi watakiwa kujisalimisha na kufuata taratibu za kisheria kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwabaini wote na kuwachulia hatua kali za kisheria ikiwa sambamba na kuwafikisha mahakamani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara alipokuwa akiongea na wananchi pamoja na wavuvi wa kitongoji cha kisiwa kidogo Ghana kata ya Ilangala wilaya ya Ukerewe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema awawezi kukimbia wajubu wao, hivyo wahamiaji hao wajitokeze kabla hawajakamatwa, wanapokimbia huko kwao wanakimbilia visiwani wakihitaji kuishi nchini wafuate taratibu zote na wataishi wa amani.
Pia aliwataka wananchi hao kuacha tabia ya kujifanya waungwana kwa kuwakaribisha wageni hao wasiokuwa na vibali hivyo watambue hiyo ni hatari na siku wakibainika sheria nayo itawaingiza hatiani.
“Hapa Gana wahamiaji haramu wanapependa sana mtu akisha kurupushwa huko Burundi au Rwanda kituo cha kwanza ni Gana na nyinyi waswahili wanafiki kwa kujifanya waungwana mnawakaribisha mjue hiyo ni hatari inawakabili siku za usoni taarifa zote tunazo”alisema Mongella.
Aidha Mongella ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa uongozi wa kijiji hicho kuandaa taarifa ya mapato na matumizi baada ya kuonekana ubadhilfu wa fedha za wananchi za kuchangia shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Cornel Magembe akizungumzia changamoto ya viongozi wakijiji kuwa na malumbano aliitaka kamati ya siasa ya kata hiyo kupata taarifa ya kuwajadili mwenyekiti wa kitongoji na wakijiji kwa sababu hawawezi kufanya kazi na watu wenye maslahi yao binafsi .
“Tunahitaji taarifa ya hawa watu wawili,hatuwezi ukakaa na watu ambao sisi tunakazana kwenda mbele wao wanapigana kwa maslahi yao binafsi tutakapobaini mmoja wao ana matatizo tutamuondoa tutaleta mwingine na atachaguliwa hapa”. alisema Magembe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.