• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Ukerewe District Council
Ukerewe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
        • Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
        • Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Maji
    • Uvuvi
    • Kilimo na Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Ongoing Projects
    • Miradi Iliyo kamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Sheria Ndogondogo za Halmashauri
    • Fomu za Maombi
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa kwa Umma
    • Video

UKEREWE KUNUFAIKA NA AJIRA ZA WALIMU

Posted on: January 8th, 2021

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ndugu Gerald G. Mweli (Anaye shughulikia Elimu) Leo amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa katika kata na vijiji mbalimbali na kufurahishwa na miradi hiyo ambayo yote inaonesha thamani halisi ya mradi. Lengo la ziara likiwa ni kutembelea na kukagua miradi ya maenendeleo na kuzungumza na walimu wakuu, wakuu wa shule na maelekezo kuelekea kupokea ajira mpya zaidi ya 5000 watakao pangiwa katika shule mbalimbali nchi.

Mhe Mweli amesema Serikali hii inayoongozwa  na Mhe  John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko makini kuhakikishisha kuwa walimu wanapatiwa miundombinu wezeshi ili kurahisisha na kutatua changamoto zinazowakabili, ndio maana  Serikali inatarajiwa kuajiriwa walimu 5000 ambao kila mwalimu atapangiwa kituo cha kazi moja kwa moja na kati ya walimu hao wapo watakao pangiwa vituo vya kazi katika  Wilaya ya Ukerewe.

Tathimini ilifanyika mwaka jana 2020 na ilibainika kuwa kila shule inauhitaji na tulipata takwamu halisi za shule hizo pamoja na za walimu ikiwa ni pamoja na taarifa za mwalimu husika, umri, kituo cha kazi alipo na taarifa zingine. Kupitia mfumo huu wa ajira za waalimu kila mwombaji alikua na nafasi ya kuchagua shule moja kwa moja kulingana na uhalisia na uhitaji wa walimu katika shule ndani ya wilaya husika.


Lengo la kutumia mfumo huu kwa waalimu kuomba kazi ni kuondokana na kabisa na malalamiko ya walimu kuajiriwa na baada ya muda mfupi kutaka kuhama.

Mweli amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu kata kuwapokea vema walimu watakao pangiwa kuja katika Wilaya ya Ukerewe na kuhakikisha wanakuwa wanapata mazingira rafiki ya wao kuendelea kuwepo na kuwa na shauku ya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.


 Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe amewapongeza waalimu wote kwa ujumla katika wilaya ya Ukerewe kwa juhudi wanazoendelea kufanya katika kunyanyua hali ya elimu kwani ni kwa miaka miwili mfululizo matokeo ya mitihani Wilaya imeshika nafasi ya nne (4) kati ya nane (8) kimkoa.


Magembe amewasihi kuhakikisha kuwa walimu wote watakao pangiwa kujakufanya kazi Ukerewe watakutana na mazingira rafiki ya wao kuishi na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. “ mazingira yetu sio mabaya kama wengi wadhaniavyo bali ni kwasababu tu tupo kisiwani”


Nae Ester A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe na Idara za Elimu Msingi na Sekondari  ameahidi kuendelea kushirikiana na walimu wakuu, wakuu wa shule na maafisa elimu kata kuwa walimu wote watakao kuja ukerewe watakua na mazingira mazuri ya wao kufanya kazi.

Matangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2021 BWENI NA KUTWA December 18, 2020
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA April 10, 2020
  • TANGAZO LA USAILI NA ORODHA WALIOITWA USAILI October 13, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA December 08, 2020
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • DKT. GWAJIMA FUATENI MAADILI YA SEKTA YA AFYA

    January 13, 2021
  • UKEREWE KUNUFAIKA NA AJIRA ZA WALIMU

    January 08, 2021
  • MADIWANI WALA YAMINI TAYARI KUWATUMIKIA WANANCHI

    December 04, 2020
  • 78 WAHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA

    November 09, 2020
  • Angalia Zaidi

Video

FURSA ZA UWEKEZAJI UKEREWE
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Jiwe linalocheza Wilayani Ukerewe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

Tovuti Mashuhuri

  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Necta

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe. Haki zote zimehifadhiwa