Mazao yalimwayo kwa wingi katika Wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 38 japo visiwa 15 vinatumika kama maeneo ya uvuvi ni muhogo, viazi vitamu, mpunga, matunda aina ya machungwa, maembe, mananasi, mapapai, kahawa, migomba, mazao ya
|
bustani na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage, njugu mawe na kunde. Mazao mengine yanayolimwa kwa kiasi kidogo ni mtama na rosella (choya). Mazao haya yanalimwa katika eneo la Ha.33, 765.5Ardhi iliyopo ni ndogo kuruhusu kilimo cha kupumzisha mashamba. Kwa hali hiyo kilimo kinahitaji kifanyike kwa tija ili uzalishaji wa mazao uweze kukidhi mahitaji ya wananchi wote ambao kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 347,145. Zao la alizeti linatiliwa mkazo badala ya zao la pamba ambalo katikamiaka ya 1970 lilikuwa zao maarufu la biashara ambalo lilikuwa linawapatia wakulima kipato. Lakini kutokana na upungufu wa ardhi hasa ukizingatia kuwa zao hili halitakiwi kuchanganywa na mazao mengine pamoja na kushuka kwa bei, zao hili lilionekana kutofanya vizuri.
|
Idara ya Kilimo ili iweze kutekeleza vyema ilani ya Uchaguzi ya CCM ni lazima ihakikishe inatekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ili kuleta tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kuendeleza na kuboresha huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuwezesha wakulima kuwa na vyama vya ushirika vilivyo hai na vyenye nguvu ya mtaji. Aidha kuwawezesha wakulima kuunda vikundi ili waweze kuwa na umoja wenye nguvu katika kufikisha bidhaa zao katika masoko ya mazao yao. Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya Vyama Vya Ushirika 71 vilivyoandikishwa chini ya Sheria Na.6 ya mwaka 2013 ya Vyama Vya Ushirika. Idadi ya VICOBA vilivyopo ni 150. Vyama vilivyo vingi vinakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea vyama hivyo kutofanya vizuri. halmashauri inakabiliwa na upungufu wa wataalam 4 wa Ushirika kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mahesabu. Ili haya yaweze kufanyika kwa ufanisi Maafisa Ugani wanatakiwa kuboreshewa mazaingira yao ya kufanyia kazi. Maboresho hayo ni pamoja na kupatiwa nyumba za kuishi katika maeneo yao na kuwezeshwa vyombo vya usafiri hususani pikipiki ili kuwawezesha kuwafikia wakulima kwa urahisi na kwa muda muafaka pale huduma za ugani zinapohitajika.
Pamoja na Serikali kutilia mkazo juu ya kilimo cha umwagiliaji wakulima bado wanategemea mvua katika kilimo. Hii ni kutokana na kutokamilika kwa miundo mbinu ya umwagiliaji katika skimu za Bugorola na Miyogwezi. Miradi hii imekwamakukamilika kutokana na ukosefu wa fedha licha ya Ofisi hiyo ya Umwagiliaji |
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.