Utaratibu wa Kupata Kibali cha Ujenzi (Building Permit)
Mmiliki kiwanja awe na Mchoro wa Ramani kutoka kwa Mchoraji anayetambulika Kisheria
Ramani hiyo ithibitishwe na idara zifuatazo:
Ofisi ya ardhi Wilaya
Ofisi ya Mhandisi wa Ujenzi Wilaya
Ofisi ya Usafi na Mazingira Wilaya
Baada ya hatua hizo mmiliki atarudi kwa afisa ardhi akiwa na ramani zilizo thibitishwa kama ilivyo elezwa hapo juu na kujaza fomu ya kupewa kibali cha ujenzi.
Baada ya kujaza Fomu Afisa Ardhi atampa Kibali cha Ujenzi.