Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Kanali Denis Mwila akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Leo wametembelea kisiwa cha Irugwa katika kata hiyo yenye vijiji viwili vya Sambi na Nabweko dhumuni likiwa ni kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo iliyopo kisiwani ambayo ni takribani zaidi ya saa sita kufika kutoka Nansio.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya Msingi Buluza iliyopewa Tsh 10,000,000.00. Kwa ajili ya ukamilishaji darasa moja ambalo mpaka sasa Ukarabati unaendelea. Kanali Mwila ameelekeza ukamilishaji umalizike haraka na Amewapongeza wananchi katika kisiwa cha Buluza kwa kujenga Madarasa matano kwa Nguvu za wananchi na ofisi mbili ambazo bado zinajengwa na sasa zipo hatua ya lenta.
Shule shikizi Lyegoba (mbinguni) Madarasa manne yaliyotolewa jumla ya Tsh 80,000,000.00 Ujenzi unaendelea hatua ya msingi (Hardcore) Kanali Mwila ameelekeza wasimamizi waongeze kasi kwani madarasa hayo yanatarajiwa kutumika mapema iwezekanavyo.
Kanali Mwila amekagua Zahanati ya Kulazu na Shule ya msingi Kulazu iliyopo Kisiwa cha Kulazu Ambapo alibaini uhitaji wa watumishi wa zahanati na kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ameahidi kufanyia kazi ikiwa ni pamoja kupata Mtumishi katika zahanati hiyo.
Katika hatua nyingine Kanali Mwila amekagua Mradi wa maji Irugwa unaotekelezwa na Wakala wa Maji vijijini (RUWASA) wenye thamani ya Tsh. 584,000,000.00 Ambapo unatarajiwa kunufaisha watu 9000 Chanzo cha maji kimejengwa kijiji cha Sambi na kusambaza katika vituo vya kuchotea maji 18.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Kanali Mwila azungumza na wananchi wa Kata ya Irugwa katika Mkutano uliofanyika Shule ya Sekondari Irugwa na wananchi walipata nafasi ya kusema kero zao.
Deus Magoma mkazi wa Kijiji cha Nabweko ameomba vituo vya maji kufika mpaka kitongoji cha Murutanga. Nae Datius Burchardi Kaimu Meneja wa RUWASA Ukerewe Ameeleza kuwa mradi ulilenga kukarabati chanzo, tanki, vituo 18 na mpaka sasa nyumba ya pampu choo na bomba zipo site na bado kulaza bomba. Ruwasa inaendelea kupitia vituo vyote na kuongeza vituo zaidi kwa kukabati vituo vilivyopo.
Bw. Daniel ametaka kuhakikishiwa kama ujenzi wa Kituo kipya cha afya au kuboresha zahanati iliyopo kijiji cha Sambi kuwa Kituo cha afya.
akijibu hoja hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Emmanuel Sherembi amesema Irugwa inaundwa na sambi na nabweko kwanini tuvutane na vyote vinaletwa kwa ajili ya Irugwa. Fedha hii ya tozo za mawasiliano ineletwa kwajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Irugwa kipya nasio upanuzi wa zahanati.
“awamu ya kwanza tumepokea Milioni 250 na tunatarajia kupokea fedha zaidi katika awamu ya pili”. Aliongeza Sherembi.
Filemoni Ladslaus mkazi wa kijiji cha Nabweko Amshukuru Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kufika Irugwa kwa Mara ya kwanza na kujionea shughuli za Maendeleo katika kisiwa hiki. Ombi lake ni kuongezewa Bweni kwani wanafunzi wamefaulu wengi hivyo kuna uhitaji wa Bweni na ameomba Shule hii iwe na Kidato cha tano na sita.
Akijibu hoja hiyo Kanali Mwila amesema Kuanzishwa kwa Kidato cha tano na sita ni jambo zuri na muhimu hivyo taratibu zifuatwe kupitia Idara husika Na Suala la Bweni ni muhimu naomba muanzishe mchakato Wake.
Akitoa msimamo wa Serikali kuhusu wapi Kituo kipya cha Afya kitajengwa Irugwa Kanali Mwila amesema Kituo hiko kitajengwa katika kijiji cha Nabweko. “Ujenzi huu umelenga kuhudumia wananchi wa Irugwa na sio sambi pekee au nabweko pekee hivyo tuache mivutano tuijenge irugwa”. Alisema Kanali Mwila.
Irugwa imenufaika na hela za Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi y uviko19 katika Shule ya Sekondari Irugwa Madarasa sita tsh 120,000,000.00 na Shule shikizi ya Lyegoba Madarasa manne Tsh 80,000,000.00 kwa Wilaya sasa tutaletewa Bilioni 3.5 kuboresha hospital ya Wilaya Nansio kuwa hospital ya Rufaa ya Mkoa.
Madarasa yanayojengwa yatakua ni yakisasa vikiwa na umeme, vigae na miundombinu yote ya Muhimu kikubwa wananchi tuendelee kuchangia nguvu ili kubakisha Fedha zitakazotumika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Shule kama vile choo.
Mhe. Joseph Sabato Msita Diwani kata ya Irugwa amshukuru sana Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na kamati ya Ulinzi na wataalamu waliofika Irugwa kuangalia utekelezaji wa Miradi yote kisiwani hapo.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.