Meli ya abiria ya MV.NYERERE ifanyayo kazi katika ziwa Victoria Wilayani Ukerewe katika kisiwa cha Ukara leo mnamo saa nane mchana imepata ajali na kupinduka. Ajali hiyo imetokea umbali unaokadiriwa kuwa wa mita 150 kufika katika katika nchi kavu.
Mv. Nyerere inafanya safari zake katika eneo la Bugorola na Ukara imepinduka na inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya mia moja (100) walio kuwepo katika meli hiyo. Hii ni kwa mujibu wa TAMESA Mwanza.
Taarifa zaidi itatolewa kwani uokoaji wa miili unaendelea mpaka usiku wa leo watu walio okolewa wakiwa hai ni 32 na walio okolewa wakiwa wamekufa ni watu 44. Alisema John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.