Baraza la waheshimiwa madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe limepitisha mapendekezo ya mpango na Bajeti ya kukusanya na kutumia jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 55,617,500,000 .00 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026/2027 .
Katika mchanganuo wa bajeti hiyo shilingi Bilioni 2,167,103,000.00 ni matumizi mengineyo kwa fedha za ruzuku ya serikali kuu, 2,246,507,400.00 ni fedha ya makusanyo ya mapato ya ndani, mapato lindwa 810,850,000.00 na 1,497,671,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayoleta jumla ya mapato ya ndani kuwa Bilioni 4,555,029,000.00 sambamba na 37,193,256,000.00 fedha ya ruzuku ya mishahara kutoka serikali kuu na 13,199,783,600.00 fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkutano huo wa baraza umefanyika leo Januari 29, 2026 katika ukumbi wa Halmashauri ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe. Ramadhan Salum Mazige.
Aidha katika mwaka wa fedha 2026/2027 Halmashauri imepanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali:
1. Kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuimarisha makusanyo ya vyanzo vilivyopo na kuongeza vyanzo vipya.2. Kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji 3. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii4. Kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara, chakula, kuimarisha uvuvi na ufugaji endelevu.5. Maswala mtambuka kama vile unyanyasaji wa kijinsia,VVU/UKIMWI,dawa za kulevya,lishe, mazingira n.k
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.