Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe limefanya vikao vyake vya kisheria kujadili taarifa za kamati katika robo ya nne. Kikao kilichofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha, Makamu Mwenyekiti pamoja na Katibu wa Kikao hiko ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Ester A. Chaula.
Akiwasilisha taarifaya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Bukindo Mhe. Gabriel K. Gregor ameeleza kuwa Halmashauri iliweka lengo la kukusanya Tsh 1.384 bilioni kupitia vyanzo vyake vya ndani lakini kufikia june 2019 halmashauri imekusanya Tsh 1.361 ambayo ni sawa na asilimia 98.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha amesema halmashauri ni tajiri sana ila inatupasa kuongeza nguvu katika kukusanya zaidi ili kuweza kuwahudumia wananchi. Ushuru wa matunda, ushuru wa hoteli, leseni za biashara pamoja na leseni za samaki zikisimamiwa vyema pato la halmashauri litapanda maradufu.
Ester Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema jitihada za kuongeza makusanyo ya ndani zinaendelea kufanyika, kwani mpaka sasa kuna kamati za mapato zimeundwa upande wa menejimenti na kushirikiana na doria ya Mkuu wa Wilaya hivyo ni matumaini yetu zitakomesha upotoshaji wa ushuru katika maeneo mbalimbali. Maeneo nane yametengwa ujenzi wa maeneo kwaajili ya kupimia samaki yameanza kujengwa na yapo katika hatua mbalimbali, pia wakusanya mapato wanamizani kwa ajili ya kupimia samaki wakati wakukatisha ushuru wa mazao ya majini.
Makatibu wa vyama ambavyo ni CCM na CHADEMA wapongeza kwa jitihada ya kukusanya na imewataka wataalamu kubuni vyanzo zaidi ili viweze kuongeza pato la Halmashauri. Wametoa pongezi kwa kamati ya fedha, utawala na mipango na menejimenti, kamati ya ulinzi na usalama kwa jitihada hizo, wamependekeza mikakati zaidi inahitajika ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amefanya ziara ya siku moja wilayani Ukerewe na kutembelea msitu wa Rubya kukagua shughuli za maendeleo katika eneo hilo. Mabula alipata nafasi ya kuzungumza na waheshimiwa madiwani pamoja na watumishi wa ardhi.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Pachal Malecha amesema idara imeandaa michoro miwili ya kutenga maeneo ya uwekezaji ya mipango miji yenye jumla ya viwanja 443 katika kituo cha biashara Bugorola hivyo jumla ya viwanja 11 vimepimwa kwa ajili ya maeneo ya viwanda, maeneo 246 ya taasisi za umma yamebainishwa kwaajili ya upimaji na mpaka sasa maeneo 29 yamepimwa. Idara inakabiriwa na upungufu wa wataalamu 15 na baadhi ya vitendea kazi kama magari.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akizungumza na watumishi wote, pamoja na madiwani ameeleza kuwa idara inapaswa kuongeza juhudi katika kupima viwanja vyote kwani Wilaya ya Ukerewe hasa eneo la nchi kavu sio kubwa sana. Amesema wizara inapitia ikama ya watumishi hivyo wapo watumishi wa ardhi watakaoletwa na hivyo upungufu wa watumishi utapungua kwa kiasi kikubwa. Upimaji ufike mpaka katika visiwa kama Ukara na vyote watu wanapoishi alisema Mabula.
Mabula amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha kuwa bajeti inatengwa na kuiwezesha idara hiyo kufanya kazi yake kwa ufanisi na kwa kasi zaidi. Amewataka kushirikiana na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya katika kutatua migogoro.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.