Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe limepitisha Tsh Bilioni 45,466,478.00 ikiwa ni makadirio ya mapato ya mwaka 2018-2019, fedha hiyo imepitishwa katika kikao cha baraza maalumu la bajeti lililofanyika katika Ukumbi mkubwa wa Halmashauri na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha na Makamu Gabriel K. Graygor na Katibu wa kikao hiko Mkurugenzi Mtendaji Frank S. Bahati.
Baraza maalumu limelenga kuhakikisha kuna uelewa wa pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi wa Ukerewe kwa kupitisha bajeti ya mwaka 2018-2019 ambapo kupitia fedha hizo wananchi watanufaika na miradi ya maendeleo. Halmashauri ya Wilaya imelenga kukusanya kiasi hiko kutoka katika vyanzo vya ndani, serikali kuu na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kawaidi na miradi ya maendeleo, alisema John Msafiri Afisa Mipango wa Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji Frank S. Bahati alisema kuwa Katika kutekeleza na kuhakikisha adhma ya Serikali katika kuwahudumia wananchi imelenga kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kwa wakati na kuanza kufanya kazi ili kuleta matokeo chanya kwa jamii. Ameahidi kuhakikisha mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Bwisya unaoendelea wataalamu wanafanya kazi kwa bidii na kuukamilisha kwa wakati.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha amewataka wataalamu kuhakikisha wanajituma ilikuwaletea maendeleo wanaukerewe na pia ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani wote kutoa maoni ya miradi ya kimkakati ambayo ipo katika maeneo yao na ambayo itawezesha Halmashauri ya Wilaya kuweza kujiendesha na kupunguza utegemezi Kutoka Serikali Kuu.
Focus Majumbi Katibu Tawala wa Wilaya ametoa wito kwa Halmshauri kuongeza nguvu katika kuibua vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha vilevilivyopo katika Wilaya ya Ukerewe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.