Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania leo imetoa hundi ya Tsh 200,000,000/- kwa kikundi cha Ushirika cha BUKASIGA kutimiza malengo yao kwa kujenga kiwanda cha barafu. Shughuli ya makabidhiano ya hundi iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Japhet Justin na kukabidhiwa kwa kikundi na Mhe. Abdalah Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi imefanyika katika kata ya Kakukuru.
Bw. Japhet Justin Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo amesema kuwa sekta ya uvuvi ni mihimu sana kwani imenatoa ajira nyingi kwa watu. Bukasiga waliandika andiko na kuomba pesa na kubadilisha maono yao kuwa vitendo na kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao ya samaki. "Naamini wakifanya vizuri benki yetu haitosita kuwaongezea fedha". Alisema Justin.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Bi. Ester Chaula ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Benki ya Kilimo kwa kukitambua kikindi hiki na kukipatia mkopo. "niahidi kwamba malengo ya kikundi yatafikiwa na tutakuwa pamoja na halmashauri itatoa wataalamu wawili wa Uvuvi na fedha watakao fanya kazi bega kwa bega kufikia malengo yao". Alisema Chaula.
Mhe. Abdalah Ulega Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi amewapongeza Bukasiga kwa kuunda vikundi cha Ushirika na sasa wanaanza kunufaika kwani wanakwenda kujenga kiwanda cha barafu na kukausha dagaa ambazo zilikua zinaharibika wakati wa mvua za masika. Adhma ya mhe Rais wetu Dkt John Magufuli ni kuwa na viwanda hakika inakwenda kutimia Ukerewe. "tunampongeza sana Rais wetu kwa kuwajali wavuvi na kuhakikisha ustawi katika sekta hii kwa kutoa mikopo kupitia benki aliyoianzisha" alisema Ulega.
Ulega amehimiza wavuvi kuunda umoja wao na kuwa na vikundi kama Bukasiga na wataweza kukopeshwa ili kuongeza tija katika uvuvi.
Josephat Mazula Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe ameshukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuwezesha ustawi wa wavuvi kwa maendeleo ya Wilaya ya Ukerewe.
Bukasiga imejipanga kutumia vema fedha hizo kwa kuhakikisha wanajenga kiwanda cha barafu kwa uhitaji wa barafu katika shughuli za uhifadhi wa samaki baada ya kuvuliwa ni mkubwa sana. Alisema Jumbula Lugola Makamu Mwenyekiti wa Bukasiga.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.