"..Jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 39 kutoka serikali kuu kupitia miradi ya kimkakati kimeshaanza kujenga hospitali kubwa katika kijiji cha Bulamba ndani ya kata ya Bukindo yenye hadhi ya rufaa hapa kwetu Ukerewe.."
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde Christopher E. Ngubiagai alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Ngoma katika mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara zake wilayani humo kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Cde.Ngubiagai amewataka wananchi wake kuacha imani potofu zinazogharimu vifo vya wengi .
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuboresha sekta ya afya kwa kujenga hospitali mpya, kukarabati miundo mbinu mbalimbali na kuongeza vifaa tiba na dawa.
"..kina mama kujifungulia majumbani acheni, hakuna sababu ya kuendelea kufanya hivyo kwa sababu hali hiyo inahatarisha usalama wewe na mtoto na sisi tunawahitaji wote muendelee kuwepo mkiwa na afya njema.." amesema Cde. Ngubiagai
Dkt.Charles Mkombe ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe yeye anapongeza wananchi kwa kuendelea kuhamasika kupata huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma hizo vilivyopo kwenye maeneo yao.
".. Tayari tumekwisha pokea milioni 250 awamu ya kwanza kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya Hamkoko iliyopo hapa kata ya Ngoma kupanda hadhi na kuwa kituo cha afya.."
Verediana Fabian ni mjumbe wa serikali ya kijiji cha Muluseni yeye anashukuru kwa huduma za afya zinazoendelea kutolewa kijijini hapo huku akipongeza mpango wa serikali kufanya ukarabati wa zahanati ya Mkoko iliyopo jirani na kijiji chao cha Muluseni.
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.