Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estomihn F. Chang’ah amefungua mafunzo ya jeshi la akiba la mgambo. Jeshi la akiba la mgambo linaendesha mafunzo ya wilaya ambapo yanafanyika katika maeneo mawili ambayo ni Masonga kata ya Kakukuru na Bukindo kata ya Bwiro. Katika ufunguzi huo akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Chang’ah amewataka vijana hao kujituma na kupata mafunzo hayo kwani ni muhimu sana kwani wananchi wametambua maana ya ulinzi na usalama kwa kukubali vijana kujiunga na jeshi la akiba la mgambo. “Huo ni uzalendo” Chang’ah. Amehimiza kuwa kazi ya ulinzi wa amani ni kazi ya askari jeshi, polisi,magereza bali amesisitiza kuwa hiyo ni kazi ya kila mtu hivyo amewapongeza sana kwa kujitoa.
Ametoa wito vijana wote waliokimbia jeshi hilo la akiba la mgambo kurudi kwani zipo faida nyingi sana la mafunzo hayo kwani yatawafanya wawena mazoezi yatakayowawezesha kujilinda na kulinda jamii, pia watapata cheti ambacho kitawasaidia kupata nafasi za kazi.
Sgt. Fales Washairi ni Mshauri wa Mgambo wilaya ameeleza kuwa mpaka kuna makundi mawili yanayopata mafunzo ambapo Masonga Kakukuru wapo vijana 132 na Bukondo wapo vijana 106 hivyo kufanya jumla ya vijana wataakao pata mafunzo hayo kuwa ni 238 ambayo ni idadi nzuri ulinganisha na mgambo 30 walio kuwepo awali.
Washairi amesema mafunzo hayo yameanza tarehe 22/6/2017 na yataendeshwa kwa wiki 16 mfululizo na yatahusisha mafunzo ya zimamoto, mafunzo ya kupambana na kuzuia rushwa, afya na uzalendo.
Chang’ah amepongeza sana kwani wilaya imefanikiwa kuvuka lengo la kuwa na jeshi la akiba lenye vijana 238 ambapo mkoa ulitaka wasiwe chini ya vijana 200.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.