Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh F. Chang’ah amepiga marufuku hiyo katika mkutano wa hadhara alipo kuwa akiongea na wananchi wa Nansio mkutano uliofanyika eneo la stendi ya zamani, mkutano ulimhusisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndugu Frank S. Bahati na Mwenyekiti wa Halmashauri George M. Nyamaha.
Chang’ah katika hotuba yake mbali na kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama ambapo aliweka bayana kuwa kuna uwepo wa wageni wasio fahamika na kutokuwepo katika daftari la wakazi. Hivyo ataanza ukaguzi na amewaagiza maafisa tarafa, watendaji wa kata na kijiji kuhakikisha wageni wote majina na taarifa zao zinafahamika.
Chang’ah alibainisha mambo makuu mawili ambayo atayashughulikia ambayo ni mimba kwa wanafunzi na uvuvi haramu. Katika msako uliopita ilibainika kuna wanafunzi zaidi ya 100 walipata ujauzito, ijapokuwa tatizo kesi hizo za mimba zinakosa ushahidi kwani wazazi wanapoteza ushahidi kwa kushirikiana na watuhumiwa. Hivyo Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na vyombo vya dola na Mkurugenzi mtendaji watahakikisha watuhumiwa wote wanachukuliwa hatua za kisheria.
Ametoa rai kwa wavuvi wanafanya shughuli ya uvuvi katika ziwa victoria hasa upande wa Ukerewe kuachana na kujihusisha na matumizi ya zana haramu za uvuvi kwani unaharibu mazalia ya samaki ziwani hivyo serikali hivi karibuni itafanya msako mkubwa ili kutokomeza tabia hiyo. “Wote wanaojihusisha na uvuvi wa kutumia zana haramu za uvuvi kukiona cha mtema kuni” alisema Chang’ah.
Chang’ah ametaka utekezaji wa nyavu(zana za uvuvi) zitakazo kamatwa lazima wahusika wachukuliwe hatua za kisheria. “ukitaka kuishi kwa amani na raha katika serikali ya awamu ya tano fuata sheria, kanuni na taratibu za nchi” Chang’ah.
Chang’ah amewataka wananchi hususani vijana kuachana na tabia ya ukaaji vijiweni badala yake wajishughulishe kwa kufanya kazi ili kuweza kujipatia kipato kwani imeonekana wazee na wamama ndio wanajishughulisha katika maeneo mengi ya wilaya wakati vijana wanacheza “pool table”. Amekemea tabia hiyo na kuwataka kufanya kazi mbalimbali kama biashara na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia fursa ya kuzungukwa na ziwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe Frank Bahati amekanusha dhana iliyojengeka miongoni mwa watu kuwa Ukerewe ni masikini hivyo ametoa rai wananchi kutoa ushirikiano kwa kulipa ushuru ila kuinua mapato na amesema mfumo wa ukusanyaji mapato utaimarika ili kudhibiti maeneo yote yenye mianya ya upotevu wa mapato.
Bahati alisema halmashauri imebuni miradi ya uvuvi endelevu kwani soko kubwa la samaki na dagaa litajengwa katika eneo ka Kamasi ambapo hekari 14 tayari zimepatikana kwaajili ya ujenzi huo na soko hilo litatoa fursa kwa wafanyabiashara kwenda kununua samaki hivyo kumuongezea mvuvi tija. Pia itaenda sambamba kabisa na uvuvi wa kisasa zaidi yani uvuvi wa kitalu ambapo mpaka sasa mchakato upo wizarani tayari kwa taratibu zingine.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Nyamaha ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano pamoja na baraza la madiwani katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo katika Nyanja zote na alibainisha changamoto ya iliyopo katika mabucha yaliyopo sokoni Nansio na kuwaondoa hofu wafanyabiashara hao kuwa ni ya serikali ni njema na kwa sasa ramani mpya ya vibanda vya soko kuu la Nansio imekamilika.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.