Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh Chang'ah leo amezindua zoezi la upigaji dawa katika mazalia ya Mbu ambao ndio chanzo kikuu cha ugonjwa wa malaria. Uzinduzi huo umefanyika Kata ya Kagera,kitongoji cha Mviringo na kuhudhuriwa na wananchi waliojitokeza kupata elimu ya namna bora yakuzuia na kuharibu mazalia ya mbu waenezao malaria. Chang'ah amewataka kila kijiji kuchagua mtu mmoja ambae atasimamia upigaji dawa hiya na amewataka watu kuacha tabia ya kutumia neti za kulalia kufugia kuku na ameagiza viongizi wote kufanya ufuatiliaji wa neti zote zilizogawiwa kwa wanawake wajawazito na wale wenye watoto watakao bainika kitumia vinginevyo wachukuliwe hatua.
Amewataka kutunza mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu.
Dkt. Kombe Nyanda Kaimu. Mganga Mkuu wilaya amewaondoa hofu watu kuwa dawa hiyo sio sumu na haina athari kwa viumbe hai vingine na imetengenezwa nchini na nikwaajili ya vimelea vya Malaria tu.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.