Kampuni ya soda ya Cocacola imekabidhi vifaa vya michezo katika shule zote za sekondari Wilayani Ukerewe, ambapo Mwakilishi wa kampuni hiyo Maulid Juma amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Frank S. Bahati vifaa hivyo.
Juma amekabidhi vifaa vya michezo kwa shule 25 za sekondari, vifaa hivyo ni pamoja na mipira 25, Jezi 31 za rangi nyekundu, nyeupe na nyeusi. Vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kutumia katika mashindano mbalimbali yatakayofanyika ndani ya wilaya au mkoani, alisema Juma.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Frank Bahati amewataka walimu wote wa michezo katika shule zote zilizokabidhiwa vifaa hivyo kuthamini mchango wa kampuni ya Cocacola ambao ni wadau wa wakubwa wa michezo, hivyo amehimiza utunzaji wa vifaa hivyo kwani vitasaidia kuinua vipaji vingi vya wanafunzi vilivyopo mashuleni kwani wakifanya vizuri wanawezakupata nafasi ya kuwakilisha Wilaya na hata taifa.
Bahati amesisitiza michezo mashuleni ni muhimu sana ndio maana kuna waalimu wanaosimamia michezo na kuibua vipaji vyao na kuweza kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kiwilaya, kimkoa na kitaifa. Wilaya ya Ukerewe imefanikiwa kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo UMISETA na UMITASHUNTA.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.