Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Kanali Denis Mwilla ameshiriki katika uchimbaji wa msingi wa madarasa manane (8) katika Shule ya sekondari Nkilizya Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, Kanali Mwila ame fafanua kuwa Wilaya ya Ukerewe imepokea fedha kutoka serikalini takribani kiasi cha billioni tatu ambazo zitajenga madarasa 155 ya sekondari kwa thamani ya B 3.1, madarasa manne kila shule kwa shule tatu za msingi shikizi yenye thamani ya millioni mia moja na sitini (M.160), bweni moja la watoto wenye mahitaji maalumu lenye thamani ya millioni themanini (M.80).
Kanal Mwila ameelezea changamoto iliyopo ni kukosekana kwa simenti jambo ambapo tayari ame wasiliana na mamlaka za juu ili kuharakisha uwepo wa simenti kwa kila kituo cha ujenzi ili ifikapo tarehe 15/12/2021 miradi yote iliyo ainishwa iwe imekamilika wilayani hapo.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Kata ya Nkilizya Janeth Haningtone ametoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa fedha zilizo elekezwa wilayani Ukerewe kuwa zitasaidia kutatua kero ya upungufu wa madarasa wilayani hapo, aidha amewaomba wananchi wajitolee zaidi katika shughuli za maendeleo kwa kuwa wana mchango mkubwa katika kuijenga Tanzania moja na yenye maendeleo hasa upande wa miundo mbinu ya elimu.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kitongoji Cha Kenonzo Kijiji cha nkilizya kata ya Nkilizya Bw. Vicent Mrugwa akiongozana na wananchi wake, ameelezea kufurahishwa na msaada huo wa madarasa manane katika eneo lake na kuahidi wapo tayari kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kushiriki maendeleo anayoyapeleka kwa wananchi.
Mwisho.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.