Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh F. Chang’ah ameongoza zaidi ya wanafunzi 100,000 katika zoezi wa umezaji wa kinga tiba kwa kusimamia na kukagua namna shughuli ilivyofanyika ili kuhakikisha zoezi linakamilika vizuri. Ametembelea shule kadhaa ikiwemo shule ya msingi Kagera, kakerege, Malegea na Murutunguru.
Chang’ah ameeleza umuhimu wa watoto na wanafunzi kumeza dawa hizo za minyoo na kichocho ambapo ametaja faida kuu ni kwamba dawa hizo zinasaidia kuzuia magonjwa hayo kwani inaelezwa kuwa maeneo kanda ya ziwa ndio maeneo yenye hatari zaidi kwani bado watu hutumia maji ya ziwa katika matumizi yao ya kila siku hivyo kuongeza nafasi ya maambukizi ya magonjwa hayo. “Ni muhimu kumeza dawa hizi kutokana na mazingira yetu ya ziwa kuna magonjwa mengi”, alisema Chang’ah.
Chang’ah amekanusha uvumi unaosambazwa na watu kuwa dawa zinazogawiwa zina madhara mwilini na kuzuia uzazi na kuwaeleza kuwa dawa hizo zimethibitishwa na serikali na hazina madhara kabisa.
Revocatus kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya amewaondoa hofu na kuwathibitisha kuwa zoezi la umezaji wa kinga tiba za minyoo na kichocho zinafaida kubwa mwilini na kumfanya mtoto kuwa na kinga madhubuti katika Ascarcs, strongoiloid stercolaris, minyoo ya safura, trichuris trichura.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.