Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh Francis Chang’ah ametoa pongezi hizo wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa kiwilaya lililofanyika Kata ya Ngoma, katika kijiji cha Hamkoko.
Akisoma risala fupi Ndugu Richard Kimwamu, kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi (W) amesema, Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya Vijiji 77 na kati ya vijiji hivyo zoezi la upigaji chapa limefanyika kwa vijiji 76 ambapo katika kijiji kimoja kilichosalia cha Bugorola ukamilishaji unaendelea na kufanya mpaka kufikia tarehe 31/01/2018 zoezi hili litakuwa limetekelezwa kwa kila kijiji katika Wilaya ya Ukerewe. Katika zoezi la upigaji chapa jumla ya Ng’ombe 29,169 wamepigwa chapa.
Kimwamu amebainisha baadhi ya changamoto zilizo kabili zoezi la upigaji chapa wa Ng’ombe kuwa ni pamoja na hali ya kijografia ya Wilaya kuwa ya visiwa na kupelekea ugumu katika kufikia maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Estominh Chang’ah amepongeza kwa jitihada hizo zilizofikiwa na Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuweza kufikia hatua ya mwisho kama ilivyoelekezwa na serikali kuwa zoezi kuwa limekamilika kufikia tarehe 30/01/2018. Ametoa rai kwa wananchi kutii maelekezo ya Serikali yanayohitaji ushiriki wa wananchi.
Chang’ah ameitaka Idara ya Uvuvi kuendelea kutoa elimu juu ya uvuvi endelevu, ufugaji wa samaki kwenye mabwawa, kudhibiti na kupambana na uvuvi haramu, kukusanya na mapato yatokanayo na leseni za uvuvi, ushuru wa uvuvi pamoja na mazao ya samaki.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.