Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe. Cornel Magembe amefanya ziara ya siku nne katika tarafa na kisiwa cha Ukara ambapo lengo kuu la ziara hiyo ni kujitambulisha na kuhamasisha maendeleo katika kata, vijiji na vitongoji. Katika ziara hiyo ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe Sistaimelda Lubengo pamoja na wataalamu wengine.
Magembe ametembelea vijiji nane katika taarafa ya Ukara kwa lengo la kujitambulisha, kuhimiza na shughuli za maendeleo kwenye jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, mazingira na kilimo.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Cornel Magembe amekagua miradi ya maendeleo katika kisiwa hiko ambapo katika sekta ya afya amekagua ujenzi wa kituo cha afya Bwisya na ameridhishwa na kasi nzuri ya ujenzi wa kituo hiko ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi februari mwaka huu. Pia amekagua zahanati mbali mbali ikiwemo zahanati ya Nyang’ombe ambayo haina choo hivyo amesema endapo fedha za ujenzi wa kituo cha afya Bwisya ukikamilika na pesa kubaki basi itatumika kujenga choo.
Shule ya Sekondari Nyamanga kuanza kutumika tarehe 28 januari 2019 na wanafunzi wote wanaokwenda kusoma Bwisya na Bukiko ambao ni 280 waanze mara moja kwani majengo ya Nyamanga yaliyokuwa yametelekezwa na serikali ya kijiji yatakuwa yamekamilika. “Haiwezekani wananchi mkachanga fedha zenu mkatumia nguvu zenu mkajenga madarasa halafu yakaacha kutumika haiwezekani katika serikali ya Magufuli.” Alisema Magembe.
Madarasa manne ya Sekondari ya Bukungu yakamilike kufikia 30/06/2019 na tarehe 8/07/2019 watoto wote wanaotoka Chifule na Bukungu kuanza kutumia majengo hayo na Viongozi wote walio tumia vibaya fedha za ujenzi wa Sekondari ya Bukungu milioni 24 kukamatwa mara moja na TAKUKURU kufanya uchunguzi kuwabaini wote waliohujumu ujenzi huo.
Amewataka wanaukara na vitongoji vyake kuachana na ngono zembe kwa kutotumia kinga na kupata maradhi, amewasihi watu wote kutnza mazingira ili yawatunze na kuhakikisha wanaachana na tabia mbaya yakwenda kujisaidia na kuoga ziwani kwani ndio chanzo cha magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Magembe ameagiza watendaji wa kata na vijiji kuwakamata watu wasiokuwa na choo katika kaya na kuzitoza kiasi cha 50,000/- na fedha hiyo ikatumike kujenga choo katika shule ya msingi katika eneo husika.
Ziarani ukara amehimiza wananchi kujitoa na kuwa chachu ya maendeleo na katika kisiwa hiko kijiji cha Bukiko kimefanya vizuri katika kutekeleza agizo lake la kujenga madarasa mawili kwani wao wamejenga sekondari mawili, na maabara. Amewataka vijiji vingine kama Kome kuongeza kasi ilikupunguza changamoto ya uhaba wa madarasa inayoikabili shule za msingi wilayani Ukerewe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.