Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Lucas Magembe amezindua rasmi zoezi la umezaji wa dawa ambapo linakamilika tarehe 12/08/2018 litahusisha wanafunzi wa shule za msingi na baadhi wa shule za sekondari. Uzinduzi huo kiwilaya umefanyika katika shule ya msingi Hamkoko iliyopo kata ya Ngoma. Zoezi la umezaji dawa za linahusisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule kuanzia miaka 5-14(walioandikishwa na wasioandikishwa). Pia dawa za kichocho zitatolewa kwa jamii kwa mara ya kwanza.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Revocatus N. Cleophace ametaja aina za dawa zitakazotolewa ni pamoja na dawa za kichocho na minyoo aina ya Plaziquantel 600mg pamoja na Albendazole 400mg kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule kuanzia miaka miaka 5-14. Pia zoezi la umezaji wa dawa za kichocho zitatolewa kwa jamii kwa mara ya kwanza katika kata nane (8) ambazo ni Irugwa, Bwisya, Bukiko, Bukungu, Bwiro, Kagunguli, Ngoma na Bukanda pamoja shule 125 za msingi. Pia kabla ya umezaji dawa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa wamekula chakula.
Reginald Richard ambaye ni Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ameeleza kuwa jumla ya walengwa ni 338,849 wanatarajiwa kupata dawa za kichocho na minyoo ya tumbo. Kati yao wanafunzi wa shule za msingi walioandikishwa ni 213,968 na 704 ni watoto wenye umri husika wasioandikishwa shule. Pia takribani watu 124,177 watapata dawa za kichocho kutoka kwenye hizo kata.
Mhe. Msingi ambaye ni Diwani wa kata hiyo amewataka wananchi wa kata yake kujitokeza kwa wingi kumeza dawa hizo na pia kuwaruhusu watoto wao kuja kupata matibabu. Ameeleza umuhimu wa dawa hizo kwa wananchi ukizingatia wao ndio walezi wa kuu wa wananchi. Msingi amemshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kuja kuzindua zoezi hilo la umezaji dawa kwenye kata yake na ni mara ya kwanza kiwilaya.
Magembe amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kumeza dawa hizo kwani ni mpango wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na na Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kupitia Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, imechukua hatua ya kutoa dawa za kichocho na minyoo. Amewaasa waachane na fikra potofu iliyojengeka katika jamii kuwa dawa hizo sio nzuri na zinadhoofesha mwili jambo ambalo sio la kweli. “Sio nia ya serikali kumdhuru watu wake tujitokeze kwa wingi na watoto wetu tupate kinga” alisema Magembe.
Mkuu wa Wilaya amehitimisha kwa kwenda kukagua shule zingine ili kujiridhisha juu ya umezaji wa dawa za minyoo na kichocho ambapo alikuta zoezi linaendelea vizuri na amewataka walimu wote kusimamia vizuri kwa kushurikiana na ofisi ya mganga mkuu wa Wilaya.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.