Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde.Christopher Ngubiagai, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo ndugu Vincent Augustino Mbua wakiambatana na wataalam wamefanya ziara katika kisiwa cha Ukara lengo kuu likiwa kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wa eneo hilo .
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa upanuzi wa zahanati ya Nyamanga iliyopo kata ya Nyamanga inayotarajiwa kupanda hadhi na kuwa kituo cha afya baada ya ukamilifu wa mradi Cde.Ngubiagai amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kukamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma bora za afya .
Akitoa taarifa ya mradi huo Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Paul Christopher amesema mnamo Septemba 1, 2024 walipokea milioni 527.7 kutoka serikali kuu kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mpango wa uwekezaji katika Afya ya mama na mtoto nchini.
Mradi unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji,wodi ya wazazi,"walk way",maabara, sehemu ya kufulia nguo,uwekaji maji na umeme sambamba na mfumo wa maji taka huku akibainisha kuwa ujenzi upo hatua za ukamilishaji na 80% ya fedha imeshatumika.
"Mhe.Rais anatoa fedha kwa wakati,sisi tunashindwa kutekeleza kwa wakati naomba mradi ukamilike Disemba 2025." Amesema Mhe. Ngubiagai
Nae Mkurugenzi Mbua amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu fedha hizo kufika Nyamanga na kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo kukamilisha mradi huo kwa ufanisi na haraka ndani ya muda aliogiza kwa kukabiliana na changamoto za kijografia na upatikanaji wa shida wa wazabuni kutekeleza mradi.
Mbali ya ukaguzi wa mradi viongozi hao walipata fursa ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu huku suala la Kamchape(tiba ya ki imani za jadi inayosadikika kutibu watu kimiujiza) likizua mjadala mkubwa kwa wananchi hao ambapo Cde.Ngubiagai ametoa agizo kwa Kamchape kujitokeza kujisajiri na kutambulika rasmi kwa serikali ili kuondoa manung'uniko ya wananchi kutapeliwa fedha katika mchakato wa kupata huduma hiyo.
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.