".. vyombo vya habari kwa hakika ni mhimili wa maendeleo, kupitia ninyi wananchi wanapata taarifa sahihi, serikali inasikia sauti za wananchi, changamoto za jamii zinazoibuliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.Flamingo FM sio tu chombo cha habari bali ni mshirika muhimu wa maendeleo ya Ukerewe.."
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde, Christopher Ngubiagai wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa habari katika hafla ya " Flamingo FM get together" iliyoandaliwa na kituo cha redio ya kijamii FLAMINGO FM iliyopo ndani ya wilaya hiyo.
Amewataka wanahabari kuwa daraja la kujenga uelewa juu ya sera na sheria mbalimbali zinazo tolewa na serikali kwenda kwa wananchi huku akiwahakikishia utayari wa serikali kushirikiana nao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Nae msimamizi wa kituo hicho cha redio ya Flamingo Ukerewe Ndugu Ayubu Mbasha amewakaribisha wananchi wote wa Ukerewe kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na kituo hicho.
Mhandisi Deusdedith Shinzeh ni Mkuu wa chuo cha ufundi stadi VETA Ukerewe yeye amepongeza juhudi zinazofanywa na kituo hicho cha redio za kuhabarisha umma na kutangaza fursa za uwepo wa nafasi za masomo chuoni kwake huku akisisitiza wazawa kujitokeza kwa wingi kupata ujuzi.
Aidha, Cde.Ngubiagai amewataka wanahabari kuwa wawazi na wawajibikaji katika kuhamasisha amani,maendeleo,kukuza uzalendo, kutangaza mafanikio ya serikali na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na serikali.
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.