"... elimu ndiyo maendeleo ya jamii ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha watoto wanapata elimu bora katika mazingira rafiki,tuwapatie chakula hata mlo mmoja wakiwa shuleni tushirikiane kwa pamoja kutimiza ndoto za watoto wetu na kukataa utoro ili kuongeza ufaulu na kujenga kizazi imara..."
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cde.Christopher Ngubiagai alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Kakukuru katika kijiji cha Namakwekwe-Mibungo mkutano uliolenga kusikiliza na kutatua kero juu masuala mbalimbali ya jamii uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Namakwekwe.
Cde.Ngubiagai amewahimiza wananchi hao kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo ya familia na jamii huku akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuhakikisha maeneo ya makazi yanakuwa safi, salama na rafiki kwa afya ili kujenga maendeleo endelevu .
Akieleza changamoto zinazowakabili Mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Christopher Bwanaku amebainisha upungufu mkubwa wa watumishi wa umma, kutokuwepo kwa bwalo la chakula shule ya sekondari Mibungo, mikopo kwa wazee, upungufu wa nyumba za walimu na watumishi wa afya na kumuomba kiongozi huyo alishughulikie suala hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ambaye pia ni Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Charles Mkombe amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuajiri watumishi wapya kulingana na upatikanaji sambamba na mahitaji, huku akikiri kuwepo kwa mipango ya kuboresha miundombinu ya shule kama ujenzi na ukarabati wa mabwalo ya chakula kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maendeleo.
Akijibu hoja ya mikopo kwa wazee Kaimu afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Ukerewe Bi. Consolatha Komanya amesema ipo mikopo ya 7% kwa ajili ya wazee, mikopo ya 10% kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kuwasihi walengwa wa mikopo hiyo kufuata taratibu ili waweze kunufaika .
Joyce Chibuga ni mkazi wa kijiji cha Namakwekwe ameeleza kuridhishwa kwake na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kushughulikia changamoto za kiuchumi na kijamii huku akisem
|
|
|
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.