"Serikali ya awamu ya sita inayo nia njema kabisa katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika na rasilimali zilizopo katika maeneo yao ,kazi yenu ni moja kuimarisha upendo na ushirikiano baina yenu."
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde. Christopher E. Ngubiagai alipokuwa akizungumza na vikundi ,vyama vya ushirika na watu binafsi katika kijiji cha Musozi kata ya Bukindo wanaojihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na usafirishaji kwa njia ya boti za kisasa vilivyotokana na mikopo ya Rais Samia.
Amewataka wavuvi hao kufanya kazi kwa umoja,amani na mshikamano ili kufikia malengo waliyojiwekea kwa wakati hali itakayorudisha shukrani ya aina yake kwa Rais Samia aliyeruhusu fedha hizo ziwafikie.
Takriban shilingi Bilioni 1.1 imetolewa kwa wavuvi wa Ukerewe jumla ya vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi 11 ikiwa ni miradi yenye lengo la kuimarisha hali ya kiuchumi kwa wananchi wa Ukerewe.
Silvester Lucas ni miongoni mwa wanaushirika amekiri kuwa wako tayari kutumika kama chachu ndani ya jamii za wavuvi katika kuibua miradi ya uvuvi itakayozalisha ajira kwa wananchi wengi zaidi.
Nae Mwenyekiti wa Musozi Mariculture Dr. Richard Mtesigwa ameongeza kuwa yeye na wanaushirika wenzie wote wanajivunia kuwa wazawa wa Ukerewe kwani ni fursa kubwa mno kuishi eneo lililozungukwa na maji.
" Ziwa letu shamba letu "
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.