Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh F. Chang’ah amefurahishwa na hatua nzuri ya ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana inayojengwa kwa msaada wa marafiki kutoka marekani kupitia kanisa la Africa Inland Church (AIC), amesema hayo alipokwenda kutembelea na kujionea ujenzi wa shule hiyo yenye dhumuni chanya la kusaidia watoto wakike kupata elimu.
Wazo la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana lilikuja kutoka kwa mama wa kimarekani aliyekuja Ukerewe kufanya research ya PhD mwaka jana 2016 na katika kipindi hiko alibaini changamoto ya watoto wa kike wanaoishi mbali na shule ambapo wanakutana na vishawishi na wengine kuingia katika maadili maovu na kupata mimba za utotoni. Hivyo kwa kushirikiana na kanisa la AIC Dayosisi ya Mara na Ukerewe aliweza kuwasiliana na marafiki waishio marekani ikiwemo Hunter Parker na kupata hela zilizowezesha kuanza kwa ujenzi wa shule hiyo kubwa nay a kisasa ya wasichana itakayoitwa Tumaini Jipya Girls Secondary School.
James Mnubi ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa shule hiyo amesema ujenzi utakua na awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza ujenzi utagharimu shilingi Bilioni 4, na miundombinu itakayojengwa ni Nyumba za walimu 8,madarasa 8, mabweni 4, vyoo vya walimu na wanafunzi. Ambapo mpaka sasa miundombinu iliyokamilika ni madarasa mawili, bweni na vyoo matundu saba na moja kwa wenye mahitaji maalumu, na jingo la utawala linatarajiwa kuanza na kukamilika kabla ya ufunguzi wa shule hiyo mkombozi hapo January 2018. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa madarasa kwa ajili ya kidato cha tano na sita.
Chang’ah amepongeza wadau hao wa elimu kwa hatua nzuri ya ujenzi wa shule hiyo itakayo mkomboa mtoto wa kike katika mazingira magumu ya masomo na kuwaepushia vishawishi na kuondokana na tatizo la mimba za utotoni. “Nimefurahishwa sana na hatua hii kwani sasa naamini elimu wilayani ukerewe itazidi kuinuka hasa kwa wasichana na tutatoa ushirikiano kuhakikisha lengo la elimu bora kwa wasichana linatimia” alisema Chang’ah.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.