Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndugu Vincent Augustino Mbua amefungua mafunzo ya siku 2 ya kuwajengea uwezo wakuu wa divisheni na maafisa bajeti ili waweze kuandaa mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 itakayokidhi viwango vinavyokubalika.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mbua amesema mafunzo yanayotolewa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa dira ya taifa - 2050 iliyozinduliwa Julai 2025 .
"..Moja ya nguzo muhimu katika utekelezaji wa dira ya taifa 2050 ni kuwa na mipango na bajeti inayotekekezeka.." amesema Mbua
Aidha ameainisha mada zitakazofundishwa kuwa ni pamoja na changamoto za kibajeti ambazo zimekuwa zikiathiri mipango mizuri , wajibu wa watendaji wa Halmashauri kwenye mfumo wa upangaji (PlanRep),uandaaji wa shabaha sambamba na uandaaji wa bajeti yenye mlengo wa kijinsia.
Alfred Sungura ni Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya hiyo yeye amewaasa watendaji hao kuwa na bidii katika kujifunza ili kazi ya kupanga na kufanya bajeti iwe zoezi jepesi.
Akihitimisha zoezi hilo Ndugu Mbua amewasihi wataalam hao kuandaa bajeti kwa ufanisi na weledi kwa kuzingatia kuwa mipango na bajeti nzuri ndio msingi wa maendeleo ya wananchi wa Ukerewe.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.