Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Ndugu Vincent Mbua amefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Ngoma ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa viwango vinavyokubalika.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya kata ya Ngoma katika eneo la zahanati Hamukoko ,serikali imetoa jumla ya shilingi million 250 kwa awamu ya kwanza katika mradi huo wenye lengo la kuboresha huduma za afya na kupandisha hadhi ya zahanati hiyo kuwa kituo cha afya.
Ametembelea ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Hamukoko ambapo amemsisitiza Mhandisi wa Halmashauri kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya mwezi Desemba ili niwe ikatumike kuanzia Januari 2026 wanafunzi watapo fungua shule katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa uliopo.
Amewataka wataalam na mafundi kuongeza kasi na bidii katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili kuleta tija kwa wananchi.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.