Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima Leo amefanya ziara ya kikazi Wilayani Ukerewe. Lengo lilikiwa kukagua hospitali ya Nansio iliyopandishwa hadhi na kuwa Hospitali na Mkoa ya Nansio. Ikiwa ni ufuatiliaji wa Ahadi za Serikali na na Chama zilizotolewa kipindi cha nyuma. Ahadi hizo ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Nansio ipande na kuwa Hospitali ya Mkoa na kifuatilia Maendeleo ya hospitali ya Bwisya ambayo imepandishwa hadhi na kuwa hospitali ya Wilaya. Zahanati ya Irugwa ambayo inatakiwa ipande kuwa kituo cha afya, gari la wagonjwa, vifaa pamoja na utoaji huduma.
Gwajima ameelekeza kabla ya tarehe 31 Januari timu ya wataamu wa mkoa pamoja na wizara kufika Nansio na kukamilisha zoezi la upembuzi wa kila kinachohitajika katika kuifanya Hospitali ya Nansio kuwa ya Mkoa. Pia taratibu za kuifanya zahanati ya Irugwa kuwa Kutoa cha Afya zianze mara moja na ameahidi kufanyia kazi suala la upatikanaji wa gari la wagonjwa.
“kwa hali yakimazingira Haiwezekani ukaacha kufikiria ukerewe au mafia na kuanza kufikiria Dar es salaam na hospitali za mjini kwani uhitaji uliopo kisiwani hapa ni mkubwa zaidi ukilinganisha na mjini” alisema Gwajima.
Katika hatua nyingine Dkt Gwajima amekemea tabia ya watoa huduma upande wa dawa ambao hawatoi dawa kwa kisingizio kuwa dawa hakuna wakati dawa zipo. Alibainisha haya baada ya baadhi ya wagonjwa kusema kuwa hawakupatiwa paracetamol na alipokwenda mahali pakuhifadhia dawa alizikuta dawa hizo. Amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuwachukulia hatua watumishi Sita ambao walikua na tuhuma za ubadhilifu wa dawa baada ya kulipa Milioni 100 kama fidia ambayo Mahakama iliamuru walipe.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe Cornel Magembe amewasihi watumishi wa sekta ya afya kuendelea kufuata maadili ya sekta hiyo na kuhudumia vema wananchi ili kuwa na taifa lenye afya nzuri.
Mhe. Joseph Mkundi Mbunge wa Jimbo la Ukerewe ameomba Wizara kuangalia kwa ukaribu Wilaya ya Ukerewe kwani ni moja kati y Wilaya zenye visiwa vingi na Kuna changamoto za jiografia kutokana na kuzungukwa na maji.
Dkt. Gwajima ameahidi kushughulikia changamoto zinazokabili hospitali Ukerewe na Amewapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayofanya amewataka kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kufuata taratibu, miongozo na kanuni na ueledi katika kuhudumia wagonjwa.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.