Shirika la Huduma kwa Wakulima (FFS) chini ya ufadhili wa Rotary Club wamekabidhi madawati 126 yenye thamani ya Tsh 6,250,000/- kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, hafla iliyofanyika makao makuu ya Halmashauri na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Cornel Magembe.
Mwenyekiti wa Bodi ya FFS Bw. Makubi amepongeza hatua ambayo Asasi hii kwa kuwa mfano wa kuigwa na Asasi zingine ndani na nje ya Wilaya ya Ukerewe.
Mratibu wa FFS Bw. Reuben Richard ameeleza Mradi wa kutengeneza madawati 126 umeanza mwezi oktoba 2020 na kila dawati limegharimu Tsh. 50,000/- kazi iliyofanyika katika Shule ya ufundi Bukongo.
“Madawati haya yatasaidia kupunguza uhaba mkubwa wa madawati uliopo mashuleni” Alisema Richard. Aidha Matarajio yetu ni kutenengeneza madawati zaidi ya 200 na mpaka sasa baada ya kutoa dawati 126 tumebakiza dawati 100 ili kufikia lengo kwa mwaka huu. Aliongezea Richard.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bi. Ester Chaula ameshukuru Shirika la FFS na Rotary Club kwa kuunga mkono sekta ya elimu ambayo ndio msingi kwa elimu ya mtoto.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Joshua Manumbu amepongeza mashirika hayo kwa kuendelea na wadau wazuri wa Maendeleo katika Wilaya ya Ukerewe ambapo Rotary Club wamefanya pia katika Sekta ya kilimo na maji pia.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Cornel Magembe ameshukuru wadau na Asasi hizo kwa kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma. Amewasihi Asasi zingine za kiraia kujitokeza ili kupunguza upungufu huo.
“Kuna upungufu wa madawati zaidi ya 4000 kwa Shule za Msingi na Sekondari bado tunaendelea kuhitaji wadau kutuunga mkono” alisema Magembe.
Aidha amewaomba wananchi ambao ni wazawa wa Ukerewe kuja na kuchangia miundombinu hasa ya Elimu na Afya. “nawaalika wote walioko maeneo mbalimbali mikoani na duniani kuja tushirikiane katika shughuli za Maendeleo”. Aliongeza Magembe.
Salila mfungo Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kalendelo Amesema Shule hiyo kwa kushirikiana na wananchi imejenga darasa 3 na yameezekwa. Tunashukuru kwa madawati haya yatapunguza upungufu wa dawati. Shule ya Msingi Kalendelo imepatiwa madawati 40,
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.