Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 13 Agosti 2018 amefanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bi. Esther Anania Chaula aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Uteuzi huu ni wa kwanza na wakipekee kwani ndiye atakuwa Mkurugenzi Mtendaji mwanamke wa kwanza kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe tangu mwaka 1984.
Esther A. Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe amewasili na kukabidhiwa ofisi na Mkurugenzi mtendaji aliyemaliza muda wake Frank Bahati na akizungumza na wakuu wa idara na vitengo Chaula ameomba ushirikiano kwa watumishi wote katika utekelezaji wa majukumu, na kushauriana kwa usahihi kwa lengo moja la kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwahudumia wananchi wa Ukerewe kiujumla.
Frank S. Bahati ni Mkurugenzi wa 12 ambaye amemaliza muda wake amebainishakuwa mkurugenzi mpya ni mwanamke wa kwanza kuwahi kuwepo katika halmashauri hiyo. Amesema hayo alipokua akifanya makabidhiano ya ofisi baina yake na Mkurugenzi mpya Bi. Esther A. Chaula ambaye amewasili kujakuripoti na tayari kuanza majukumu yake.
Frank S. Bahati amemkaribisha na kumtakia kila la kheri Esther A. Chaula anapokua akianza majukumu yake kama mkurugenzi mtendaji na amemtaka kuwatumia vizuri wataalamu waliopo katika ofisi yake ili kumsaidia kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Bahati ametumia fursa hiyo pia kuwaaga na kuwashukuru watumishi wote wa umma kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha uongozi ndani ya wilaya Ameyasema hayo katika ukumbi mdogo wa mikutano wa halmashauri. Bahati amesisitiza umoja na ushirikiano wakuu wa idara na vitengo walio mpatia wampe pia na mkurugenzi mpya.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.