Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameanza ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ukerewe na ametembelea Zahanati kijiji cha Sizu kata ya kagunguli na kukagua zahanati hiyo pamoja na namna huduma zinavyotolewa. Ikiwa ni mara yake ya kwanza kama Mkuu wa Mkoa kuwahi kufika katika kisiwa hiko tokea Uhuru. Ameeleza adhma yake kupitia ziara hiyo kuhakikisha anatembelea visiwa vyote vinavyounganisha kisiwa cha Ukerewe.
Elizabeth John Amos Tabibu Msaidizi wa Zahanati ameeleza kuwa imeweka mikakati ya kupunguza vifo vya wakinamama na watoto, kutoa Elimu na kutumia dawa za kuongeza Damu na kuhudhuria cliniki mapema.“Ufinyu majengo ya kutolea Huduma za Afya kwani Mpaka sasa jengo lilopo ni moja tuu, Uhaba wa watumishi ambapo kituo kinawatumishi wawili.” Alisema Elizabeth.
Mongella ameahidi kishughulikia changamoto hiyo pamoja na kupata jengo la kujifungulia Katika zahanati hiyo. Na amewapongeza watoa huduma katika zahanati hiyo kwa kuendelea kuwahudumia wananchi.
Katika shule ya Msingi Sizu Mkuu wa Mkoa amechangia kiasi cha Tsh 100,000, Tsh 50,000/- kutoka kwa afisa Elimu Mkoa, na Mkuu wa Wilaya Mhe Cornel Magembe ameahidi mifuko 10 ya saruji.
Mongella ametembelea kisiwa cha Kweru mto ambapo amekagua shule shikizi ambayo imejenga madarasa manne pamoja na ofisi ya walimu mradi uliogharimu Tsh 33,000,000/- ambapo inahusisha mchango wa Mkurugenzi, Mchango wa wananchi pamoja, NMB pamoja na mifuko 193 ya saruji fedha za Mfuko wa jimbo, katika kisiwa hiko Mongella apepongeza wanakweru mto kwa jitihada hizo na ameahidi kuwa atafuatilia madarasa mawili yaliyosalia pamoja na ujenzi wa Choo ili shule hiyo ipatiwe usajili kamili.
Mongella amefurahishwa na hali ya kujitoa ya wananchi wa kisiwa hiko katika kuchangia maendeleo yao kwa kujenga shule hiyo, hivyo ametoa ahadi ya kuchangia mabati 100 ili wakamilishe majengo yaliyosalia.
Awali mwenyekiti wa Halmashauri Mhe George Nyamaha amemweleza adhma ya wananchi wa kisiwa hiko kuwa ni kuboresha Elimu na wapo tayari kukamilisha ujenzi kwa mifuko iliyotolewa na mbunge ili kupatiwa usajili.
Akiwa Katika kisiwa cha Irugwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema atafuatilia upatikanaji wa Meli ya kubeba abiria na anaamini Mhe. Dkt John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni msikivu katika mahitaji ya wananchi. Ameeleza hayo kufuatia ombi la Mkuu wa Wilaya juu ya Adha kubwa ya usafiri wapatayo wanairugwa.
Mhe Joseph Mkundi Mbunge wa Ukerewe (CCM) amewapongeza wanairugwa kwa kutumia vema mifuko 200 ya saruji zilizotolewa na mfuko wa jimbo pamoja na miundombinu yote iliyotolewa na serikali ya awamu ya Tano.
“Pamekuwa na changamoto ya watu wengi kukosa namba za vitambulisho vya taifa, hivyo nawataka watumishi wa NIDA wilaya kutoka na kuwafuata watu na kuwapatia namba na ambao hawajaandikishwa kupatiwa huduma hivyo kufikia tarehe 14 februari.” Alisema Mongella.
Amewataka wananchi kuachana na uvuvi wa kutumia zana haramu kwani unaharibu mazalia ya samaki na hairusiwi kisheria hasa za nchi yetu ya Tanzania.
Copyright ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe . All rights reserved.